TETESI za Ujauzito wa Wema Sepetu Zawa Gumzo, Yadaiwa Hamjui Mwenye Mimba Hiyo Kama ni Idriss ama Mbunge

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Habari zinazosambaa kwa kasi ya ajabu kama moto wa kifuu zinaeleza kuwa, mtoto mzuri ndani ya Bongo Movies, Wema Sepetu ‘Madam’ mbali na taarifa za kuwa mjamzito, hadi sasa bado yupo kwenye wakati mgumu kuweza kutegua kitendawili cha nani mmiliki halali wa kiumbe kilichopo tumboni mwake, Risasi Mchanganyiko linakupa habari kamili.


Hivi karibuni, magazeti tofauti ya Global Publishers ndiyo yalikuwa ya kwanza kuripoti kuhusu uwepo wa mimba ya mlimbwende huyo asiyechuja Bongo, ambapo awali, vyanzo mbalimbali vilieleza kuwa mhusika ni mbunge mmoja machachari ambaye ndiye anayemuweka Wema mjini kwa sasa.


MAJIBU YA WEMA ALIPOBANWA
Kwenye habari ya awali iliyoripotiwa na gazeti la Ijumaa, Wema alipotafutwa kusomewa mashitaka yake kuwa ana ujauzito wa mbunge huyo, kupitia simu ya shosti wake, Aunt Ezekiel, staa huyo hakutaka kufunguka sana kuhusu mbunge huyo zaidi ya kusema; “ndiyo nina mimba, tena ya miezi sita.”

UBUYU MPYA SASA
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Miss Tanzania  huyo wa mwaka 2006 amejiridhisha kuwa ni mjamzito baada ya kupima kwenye hospitali moja maarufu (jina tunalo) na kuondoka na furaha ya ajabu lakini kitendawili alichoondoka nacho ni kuwa hamjui mhusika wa kiumbe hicho.

WOTE AWAPA ASILIMIA 50
“Madam alifurahi kweli maana suala lililokuwa linamnyima usingizi siku zote ni kutopata mimba. Baada ya furaha hiyo, ishu ikawa ni kumtambua mhusika kwani kwa nyakati tofauti ameshabanjuka kimalavidavi na mshindi wa Big Brother Hot Shot 2014, Idris Sultan na mbunge yule anayempa jeuri ya pesa kwa sasa, wote amewapa asilimia hamsini hajajua nani hasa ndiyo mhusika,” kilisema chanzo hicho.

WOTE WAWILI KAWAMILIKISHA
Chanzo hicho kilizidi kutiririka kuwa, baada ya kuona ameshachanganya madawa, Madam aliamua kila mmoja kumwambia kuwa ‘mzigo’ huo ni wake hivyo wote kwa pamoja na nyakati tofauti wanahudumia na kumjali staa huyo, tena kwa nguvu zote.
“Yaani kila mmoja kamwambia mimba yake. Wote wawili wamezipokea taarifa za ujauzito kwa bashasha huku kila mmoja akijiamini kuwa ni mhusika pasipo kujua Madam hajui nani hasa ndiye halisi.

MBUNGE, IDRISS ‘FULL’ KUHUDUMIA
“Yani ni full kuhudumia. Mbunge kwa wakati wake amekuwa akimwaga chapaa kama hana akili nzuri. Amelipia nyumba ile ya Ununio jijini Dar na kama hiyo haitoshi, amekuwa akisimamia shopping za maana tu mjini na hata ile ndiga aliyojizawadia Wema katika sherehe yake ya kuzaliwa, mbunge huyo alihusika katika malipo,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

“Idris naye si haba. Anajitutumua kwa upande wake, anaamini kwamba mzigo ni wake bila kujua mimba hiyo ina figisufigisu.”

IDRIS ASAKWA, AFUNGUKA
Gazeti hili lilimtafuta Idris kupitia simu yake ya mkononi ambapo alipopokea, alitiririka hivi:
Risasi: Mzee tumepata habari kwamba wewe ndiyo mhusika wa mimba ya Madam, vipi unazungumziaje taarifa hizo?

Idris: Kwenye hilo kwa sasa siwezi kuliongelea, labda unipe mwezi mmoja. Kichwa changu hakijatulia.
Risasi: Lakini inasemekana unagharamia kila kitu kwa sasa, ukiamini mzigo ni wako?
Idris: Aaa! Acha kuniingizia hayo mambo bwana. Wewe subiri huo mwezi mmoja ukipita nitakueleza kila kitu.

SHOGA ZAKE WAMSHANGAA!
Mashosti wake waliozungumza na Gazeti hili ambao hawakutaka kutajwa majina yao, walisema ni jambo la kushangaza kwa mwanamke kushindwa kumjua mwanaume aliyempa ujauzito.

WEMA ANASEMAJE?
Gazeti hili lilifanya jitihada za kutosha kumsaka Wema kwa kumpigia simu na kumtumia ujumbe mfupi lakini hakupokea wala kujibu ujumbe huo.

KUTOKA KWA MHARIRI
Mimba ni jambo la kheri hivyo kwa kuwa Wema ameziona simu za wanahabari wetu zikimuuliza juu ya mhusika wa kiumbe hicho, ni vyema akawapigia na kuanika kila kitu kuhusu habari hii.

CHANZO: Global Publishers (GPL)


Udaku Special Blog
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

24 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. I nshaalah atakua mtt mwema ucheke umfurahie upite ujitambe uitwe mm Fulani amini very soon

    ReplyDelete
  2. Haifichiki haina haja ya kupokea sim ya mdaku yeyote live wema I lone

    ReplyDelete
    Replies
    1. duh! kwa kingereza hicho umechemka

      Delete
    2. ndio fans wake hao, elimu darasa la saba kama yeye.

      Delete
  3. we mtoa mada unataka maadui zake wajinyonge nini? wana hasira hao subiri uwasikie makomenti yao. tehe tehe tehe hongera mama kijacho.

    ReplyDelete
  4. 😂 😂 😂 😂 😂 mtatafuta sana kupunguza furaha yake lakini ndo hivyo tena mungu amejibu nyie si ndo mlisema mgumba sasa mimba inawahusu nini mwaka huu wataisoma namba

    ReplyDelete
  5. Story of my life...she can write a book, na akawa the best seller. Zaa Wako if u can! Really?!! They have to sit down and take a time ....zaa Wako if you can! 😝 loudly, who you talking about? I mean really. Shame on you na kwa wanaume wote wanao wanyanyasa wanawake wanao ahangaika kupata watoto wakijua eti matatizo ya kupata mtoto Ni tatizo la wanawake Tu, this can be hata kwa mwanaume kuwa na matatizo yakutokuwa na uwezo WA kumpa mwanamke ujauzito,sio Tu kwa sababu Una John basi ndio Una uwezo WA kjzaa. Think twice kabla hujarusha donge, this called karma, and karma is a fucking damn bitch, I tell you...

    ReplyDelete
  6. Duh udaku bila wema haiuziki
    Kwiiiiiiii

    Kawa yy was mwanzo

    ReplyDelete
    Replies
    1. usilolijua heri upige kimya, huyu twiga ndio anao walipa wamwandike ili asisahaulike muulize yule zinjathropus imelda.

      Delete
  7. kwa sherria ya Dini ya kiislam mtoto yoyote anaezaliwa nje ya ndoa baba yake anaitwa abdallah asipate tabu kumtafuta baba yake anakuwa hana urith wowote kutoka kwa baba yake

    ReplyDelete
  8. Enter your comment...Hongera sana madam mwenyez Mungu. akujaalie mtoto mwema

    ReplyDelete
  9. mbona mond anaudumia tiffah,kna tatizo idris akiudumia?mimi nina asilimia zangu mia,tiffah si wa mond,baada ya penny kuvujisha siri,mimba alizotoa si za mond.ukitoa penny hakuna mwanamke aliyetembea na mond kushika mimba,tatizo ss watanznia ukweli atuupendi tunapenda uongo tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. tiffa ni wa mama yako tufanye, jike zima linalo bleed kila mwezi unashinda na malkia haloooooo unanukaaaaa

      Delete
  10. Hakuna mtoto haramu, kitendo ni haramu bali mtoto ni halali. Allah ampe kila la kheri Inshallah!

    ReplyDelete
  11. Pumbavu nyote
    Fyuuuuuuuuuu
    Hata mimba inatuhusu nini siye
    Tungoje azae na atuonyeshe Tumbo la mimba tuone
    Kama alionyesha uke wake jukwaani mbona haonyeshi hiyo mimba

    ReplyDelete
    Replies
    1. mchawi mkubwa weeeee.

      Delete
    2. mchawi mama yako bibi wewe unaye endekeza umalaya humjui hata baba mtoto maana hata jini lilikulala

      Delete
  12. Tusiwe Na haraka jamani mimba kamwe haifichiki tutaionaga tuu love wema forever insh itakua soon than letter

    ReplyDelete
    Replies
    1. mburula mwingine, unashindwa kumpenda mama yako unakazana njaaa kwa ngongoti asiye na time na wanuka vikwapa

      Delete
  13. Km Ni kweli am so happy with you lkn jitahidi dna muhimu ili baadae asikuadhiri mbele za watu kwa kumdai babaake

    ReplyDelete
    Replies
    1. we english yako ya toilet heri upige kiluga tu mfyuuuu

      Delete
    2. we english yako ya toilet heri upige kiluga tu mfyuuuu

      Delete
  14. HONGERA SANA BINTI SEPETU MUNGU AKUSAIDIE UJIFUNGUE SALAMA

    ReplyDelete

Top Post Ad