Dada Aliyezaniwa Msukule wa Tajiri Kibamba Anaendelea Vizuri Baada ya Kupatikana Tena Bonde la Mto Msimbazi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mariam Juma (25), maarufu kwa jina la Upa ambaye alidhaniwa na wananchi kuwa ni msukule baada ya kupatikana akiwa mtupu katika shimo lenye urefu wa futi kumi, nyumbani kwa tajiri aliyejulikana kwa jina moja la Mtei Januari 19, mwaka huu, Kibamba, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar, anaendelea vizuri kiafya katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tofauti na alivyofikishwa hapo kwa mara ya kwanza.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii wiki iliyopita, Buguruni, Wilaya ya Ilala, Issa Mohamed, mume wa Upa alisema kwamba mkewe kwa sasa anaendelea vizuri ukilinganisha na mara ya kwanza alipofikishwa hospitalini hapo baada ya kupatikana katika bonde la Mto Msimbazi maeneo ya Tabata, Januari 23, mwaka huu.

‘Msukule’ wa tajiri aendelea vizuriAidha, Mohamed aliendelea kusema kwamba Upa yupo Muhimbili katika kitengo cha watu wenye matatizo ya akili anakofanyiwa uchunguzi na matibabu na kwamba amekuwa akienda kumjulia hali na kumpelekea chakula ambapo hata yeye amekuwa akijisikia vizuri anapomuona mumewe, jambo ambalo linamfanya wale naye pamoja, kuzungumza kisha kuagana.

“Kwa mara ya kwanza alipopatikana katika shimo nyumbani kwa tajiri na kutoweka akiwa mikononi mwa polisi kisha kupatikana tena kwenye bonde la Mto Msimbazi, kuna tofauti kubwa. Namuombea kwa Mungu apone haraka arudi nyumbani kwani watoto wamekuwa wakimlilia,” alisema Mohamed.
Upa aliaga nyumbani kwa dada yake mkubwa anayeishi Tabata Matumbi, Dar mwanzoni mwa mwezi Januari, mwaka huu akidai anakwenda kuwanunulia nguo wanaye katika Soko la Buguruni lakini hakurudi nyumbani ambapo baadaye alipatikana katika shimo, nyumbani kwa Mtei.

Global Publishers
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mungu amfanyiye wepesi

    ReplyDelete
  2. Allah amfanyie wepesi ampe siha njema apate kurudi kuungana familia yake...Ameen

    ReplyDelete

Top Post Ad