Dk Phillip Mpango Akataa Kuwa Waziri OmbaOmba......Asema Serikali Haipo Tayari Kukubali Ndoa Za Mashoga Kisa Misaada Ya Wahisani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango amesema hatua ya Serikali ya kukusanya kodi kwa nguvu kwa baadhi ya wafanyabiashara waliotorosha makontena bila kulipiwa ushuru, haikuwa lengo la kumkomoa mtu, bali ililenga kukusanya fedha za Serikali yenye lengo la kuifanya nchi iache utegemezi wa wahisani.

Waziri huyo ambaye jana alikutana na makundi mbalimbali ya wafanyabiashara ofisini kwake Dar es Salaam, alisema yeye kama waziri wa fedha asingependa kuwa waziri ombaomba kwa wahisani, ambao alidai baadhi yao wana masharti magumu, ambayo hayatekelezeki kwa maadili ya Watanzania.

“Nimewasindikiza wenzangu huko nje kuomba fedha sasa nimechoka, nataka kutembea kifua mbele, maana wana masharti magumu, wengine wanataka turuhusu homosexual (ndoa za jinsia moja), masharti haya kwa kweli yanakera sana,” alisema Dk Mpango ambaye katika serikali iliyopita alikuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango.

Dk Mpango aliongeza kuwa ili nchi isonge mbele, ni lazima ikusanye kodi ya kutosha; na jana aliahidi kuchukua hatua kadhaa, zitakazoiwezesha sekta binafsi kuwa mhimili wa kuimarisha uchumi wa nchi ili kufikia malengo ya kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye kipato cha kati.

Alisema Rais John Magufuli ni kiongozi ambaye akilala na kuamka, anawaza namna ambavyo atawahudumia wananchi wake, ambao wengi wako kwenye dimbwi la umaskini.

Alisema Rais atafanikiwa tu, pale Serikali yake itakusanya kodi ya kutosha na kuwahudumia wananchi hao.

“Kuna minong’ono kwamba eti Serikali ya Awamu ya Tano inawanyanyasa wafanyabiashara wakubwa na kwamba hatua tulizochukua kukusanya kodi, ililenga kuwadhalilisha baadhi ya wafanyabiashara, hii sio kweli kabisa,” alisema Dk Mpango.

Dk Mpango alisema Serikali ya Awamu ya Tano, inatambua umuhimu wa wafanyabiashara, hivyo wizara yake itakuwa ya mwisho kuchukua hatua za kuwanyanyasa.

“Nawahakikishia kwamba nina dhamira ya dhati ya kufanya kazi kwa kushirikiana na ninyi wafanyabiashara wakubwa na wadogo ili tutimize ndoto ya Rais,” alisema.

Alisema serikali yoyote duniani ni lazima ikusanye kodi, hivyo aliwahakikishia wafanyabiashara hao kuwa kama bado kuna wafanyabiashara wanaokwepa au hawataki kulipa kodi kwa mujibu wa sheria, serikali haitakuwa tayari kuwavumilia.

Dk Mpango alisema idadi ya watu wanaolipa kodi kwa sasa nchini bado wachache, hivyo aliwaagiza wafanyabiashara wote kujisajili wapatiwe Namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN).

Pia, aliwataka waache tabia ya kufanya udanganyifu kwa kuwa na vitabu vingi vya utunzaji wa kumbukumbu za biashara. Aliwaagiza kuhakikisha wanatoa stakabadhi na suala hilo lisiwe hiyari.

“Tunajua kwamba mnatoa vitisho kwa wanunuzi kuwa kama wanataka risiti bei ni ya juu, hiki mnachofanya ni hatari kwa nchi,” alisema na kuwataka wote watumie mashine za EFD na serikali inaendelea na mpango wa kununua zingine ili wagawiwe bure.

Aliwataka kutoa taarifa kwa Kamishna Mkuu wa TRA, kama kuna mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) au wa Halmashauri ya Wilaya, ambaye atadai hongo au atawanyanyasa wakati wa kudai kodi.

Katika kutekeleza hilo, aliwapatia namba zake pamoja na za Kamishna na kuwataka waache tabia ya kutoa rushwa ili wasilipe kodi.

 Dk Mpango alisema baada ya wafanyabiashara kufanya kikao na Rais Magufuli, Serikali imeunda kikosi kazi kushughulikia kero zote, zilizotolewa na Baraza la Biashara na mojawapo ni kufuta utiriri wa kodi ili kuwapa wepesi wawekezaji kufanya biashara nchini na kumpungumzia mzigo mkulima.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Chaa kumekucha ...

    ReplyDelete
  2. Mashoga mbona wako wengi Tanzania
    Wengine wamo bungeni, serikalini? Kila kona
    Mbona wakija mashoga kwenye utaliiiiiiiii mnawapokea acheni unyanyasaji
    Ushoga si ugonjwa Upo dunia mzima

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe huna dini,maana Q imekataza na B imekataza pia.

      Delete
    2. Wewe na wenzako akina Mbatia na Kubenea ndio mnaotuharibia watoto wetu kwa kuendekeza ushoga!Hamna aibu mnalegeza hadi macho kwa wanaume wenzenu,ujinga!

      Delete
    3. CCM wajejaa mashoga tangu awamu ya pili
      Misago ndo usisime
      Kuna watu nunuliwa nyumba London Na Dubai CCM

      Delete
  3. Mungu awabariki,awatangulie kwenye kila jambo mfanyayo kwa waTZ.
    Bora ya kula majani kuliko kuruhusu ndoa ya jinsia moja.

    ReplyDelete
  4. Dr. Mpango, yuko sahihi ktk msimamo huu wa kuongeza wigo wa mapato ya serikali kupitia kodi. Bado kuna shida kwa wafanyabiashara kukadiriwa kodi kwa TRA kutumia mali/ bidhaa zilizoko dukani wakati bidhaa zilizofichwa store ni nyingi zaidi; hili hupunguza kodi.

    Sasa, tusipokuwa makini tutakusanya kodi nyingi lakini mwisho wa siku tutashindwa kuzitumia kwa ajili ya kuwaletea maendeleo kwa sababu zifuatazo:
    1. H/W ambazo ndizo agent wa kuondoa umaskini nchini kwa kuwa hupewa bajeti kubwa bado bajeti zao za mwaka zimejaa activities za "Capacity Building" - tutajengwa uwezo wa wakulima mpaka lini?
    2. Watendaji wengi wa Serikali - (RCs, DCs, DEDs, RASs) n.k kutoelewa dhana na malengo ya viongozi wa Kitaifa na hivyo kipindi rais akiagiza suala hili wao (baadhi) wanafanya lile - Mfano matumizi fedha za miradi ya TASAF III, UKIMWI, Usafi wa Mazingira, n.k bado hazisimamiwi sawia
    3. Matumizi makubwa kwenye anasa - ununuzi wa magari ya kifahali kwa Viongozi na Watendaji Serikalini (Magari tunayonunua ni ya ghali sana kwa uendeshaji wake na pale yanapoharibika. Hivyo, ilikuwa busara kutumia magari ya kawaida na haya ya kifahali tuachie wafanyabiasahra wenye fedha za kutosha;
    4. Sheria ya manunuzi nchini; hii bado ni mwiba mkubwa kwa serikali kwa kuwa mara nyingi taifa linayuba sababu ya ununuzi wa mali, bidhaa na vifaa vya serikali kuwa na bei ya juu sana - Mfano kalamu ya shilingi 100 madukani serikali inanunua shilingi 200 - 500; maji madogo kwenye mikutano yanayouzwa shilingi 500 madukani serikalini huuziwa 1,000; mikataba ya utekelezaji miradi ya maendeleo mbalimbali km maji, umeme, barabara, majengo n.k hutumia fedha nyingi sana kwa mfano nyumba ya RC, DC, DED n.k hugharimu takribani shilingi 500milioni au zaidi - kiasi hiki ni kikubwa sana

    ReplyDelete

Top Post Ad