Jose Mourinho Anatua Man United? Safari Hii Imetajwa Hadi Tarehe Rasmi …

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Stori za kocha wa zamani wa klabu ya Chelsea ya Uingereza Jose Mourinho kujiunga na klabu ya Manchester United zinazidi kushika kasi, licha ya kuwa ni tetesi hadi sasa kuhusu Jose Mourinho kurithi nafasi ya Louis van Gaal ndani ya Man United, stori hiyo inapata nguvu baada ya stori nyingi mwishoni mwa mwaka 2015 zilizoanza kuandikwa kama tetesi zote zilitimia.

Zilianza stori za Raphael Benitez kuwa atafukuzwa Real Madrid kweli stori hiyo ikawa kweli, Jose Morinho kufukuzwa Chelsea ikawa kweli, Pep Guardiola kuwa kocha wa Man City, kweli Man City wamethibitisha, stori mpya kutoka Marca gazeti ambalo stori zake zinaaminika, limetaja tarehe rasmi ya Jose Mourinho kutua Man United.

Marca wameandika kuwa Jose Mourinho atakuwa kocha mpya wa Man United kuanzia July 1 2016, licha ya kuwa Marca wanaripotiwa kuandika stori hiyo kama tetesi, lakini inapata nguvu kutokana na stori nyingi zilizoandikwa kama tetesi msimu huu zimekuwa kweli.

Gazeti la Marca linataja kuwa kama Louis van Gaal akiendelea kufanya vibaya kabla ya msimu huu kumalizika atafukuzwa na nafasi yake kurithiwa kwa muda na Ryan Giggs ambaye ni kocha msaidizi na July 1 Jose Mourinho ndio anatajwa kuwa atakuwa kocha rasmi wa Man United.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad