Sina Mpango wa Kuoa Mtu - Ney wa Mitego Afunguka..

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msanii Ney wa Mitego amesema kwa sasa hana mpango wa kuoa na wala hafikirii kuoa, licha ya kuwa na watoto ambao wanahitaji malezi ya mama.

Ney ameyasema hayo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwa sasa hayuko kwenye mahusiano yoyote, na suala la kuoa kwake ni suala zito, hivyo hawezi kukurupuka na kuchukua uamuzi wa kuoa.

"Kusema kweli kabisa nimeulizwa swali ambalo sijaulizwa muda mrefu, na nikiulizwa huwa nalikwepaga, kufuatana na mahusiano ambayo nimekuwa nayo katikati, namshukuru Mwenyezi Mungu amenijalia watoto, for this time nikisema nizungumzie kuhusu ndoa nitadanganya, mi sifikirrii kabisa kuhusu kuoa for this time, kwa bahati mbaya au mzuri mi sipo kwenye mahusiano, sitaki kukurupuka, unajua ukifunga ndoa kwa sisi, mi ni mkristo hiyo ndo nitolee, yani hapo ndo umejicomit umeshaingia kwenye 18 ambazo huwezi kuzipangua tena, sifikirii kuoa, siwazi na sidhani kama nina huo mpango", alisema Ney wa Mitego.

Pamoja na hayo Ney wa Mitego amekiri kuwa na mahusiano na Mtanzania Stella a.ka Chaga Baby ambaye anaishi Marekani, lakini umbali uliopo kati yao ndio chanzo cha wao kutokuwa pamoja.
"
Chaga baby ye yuko mbali kiukweli kabisa, labda kitu ambacho sijawahi kuzungumza kwanza kiukweli kabisa, mi nipo huku, alafu bado ana ratiba ndefu ya kuendelea kuwa kule, mi nimwanaume sitaki kuoneka mwanaume muongo ambaye anajipa matumaini ambayo hayana kichwa wala miguu, lakini wakati ukifika kama atakuja au mi nitaenda kila kitu kitakuwa sawa, but for this time niko single", alisema Nay wa Mitego.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sidhani kama kuna mwanamke anaweza kukubali kuolewa na ibilisi

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  3. Naww rukia aly au cjui ndo leila seif unatafuta kiki au?

    ReplyDelete
  4. hata huyo chaga wakiishi pamoja wataachana mwezi tu mana ww ni zigo la misumari ukilibeba kichwani ukienda nalo pole pole unaumia na ukipiga mbio linakuchoma hakuna anaeweza kukubeba baba

    ReplyDelete
  5. N.a. mambo ya kizamani hatuyataki huu wakati wa ukweli sio kuleta wizi wa kudanganya watu

    ReplyDelete

Top Post Ad