Vicent Kigosi ‘Ray’ Awacharukia Wanaosema Tasnia ya Filamu Imekufa Baada ya Kanumba Kufariki...

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msanii mkongwe wa filamu nchini, Vicent Kigosi ‘Ray’ amewataka mashabiki wa filamu kuwapuuza watu wanaodai tasnia ya filamu imekufa baada Steven Kanumba kufariki.
Ray Kigosi

Akizungumza na Bongo5 Ijumaa hii, Ray alisema huu ni wakati kwa wadau wa filamu pamoja na mashabiki kusupport wasanii waliopo kwa nunua kazi zao.

“Mimi nataka mashabiki wa filamu wajue hii tasnia inaendeshwa na wao, sisi wasanii tunategemea support yao kwa kununua kazi zetu. Mimi binafsi naukubali mchango wa Kanumba lakini ufike wakati tujue ya Kanumba yalishapita, tuwaandae akina Kanumba wengine, na wanaosema tasnia ya filamu imekufa baada ya Kanumba kufariki sio kweli na wapuuzwe.” Alisema Ray.

Aliongeza, “Mimi naamini tuna wasanii wengi wenye vipaji ambao tukiwasupport tutafika mbali zaidi. Mbona kwenye muziki leo kuna Diamond, lakini hapo nyuma kulikuwa na akina MB Dog, Matonya, TID na wengine wengi. Mimi naamini hata Diamond wakati wake ukipita watakuja wengine wakali. Kwahiyo nawaambia mashabiki wa filamu tuna wasanii wengi bado wanafanya vizuri, kinachotakiwa ni kuwasupport alafu tuone kama watashindwa.”.

Aidha, Ray amewakata mashabiki wa filamu kuisubiria filamu yake mpya ‘Tajiri Mfupi’ ambayo inatarajia kutoka hivi karibuni.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HAWANA LOLOTE WAMEBAKI KUUZA SURA NA KUTUMIKA KWENYE MAJUKWAA YA KISIASA, MOVIE ZIMEKOSA LADHA, UBISHOO MWINGI KUJIONA NA KUIGIZA MAISHA INSTAGRAM NDO KILICHOBAKI, TUTAKUKUMBUKA KANUMBA SANA

    ReplyDelete

Top Post Ad