Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda Apata Ajali Mbaya ya Gari

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mtu mmoja amefariki dunia na wengine wanne wamejeruhiwa akiwemo mke wa waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda Mama Tunu Pinda baada ya gari walilokuwa wakisafiria kumgonga mwendesha pikipiki wakati akikatisha barabara katika eneo la Mkundi barabara ya Morogoro Dodoma manispaa ya Morogoro.


Ajali hiyo imetokea majira ya saa nane mchana katika eneo la Mkundi ikihusisha gari lenye namba za usajili STK 9242 gari la mke wa waziri mstaafu Mizengo Pinda likitokea Dodoma kwenda jijini Dar-es-Salaam  na pikipiki


Majeruhi wengine wa ajali hiyo ni dereva wa gari hilo Bw Anjelo Mwisa, mlinzi wa mke wa waziri mkuu mstaafu Gaudensi Tembo na kijana wa familia ya Mama Tunu Pinda Bwana Gilbert Sampa.


Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro Dr Rita Liamuya amesema hali ya mke wa

waziri mkuu mstaafu na majeruhi wengine zinaendelea vizuri na kueleza kuwa  majeruhi hao wanatarajia kuhamishiwa jijini Dar-es-Salaam kwa matibabu zaidi
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. aliyekufa ni nani,au hana umuhimu tena?

    ReplyDelete
  2. MUNGU AWAPONYE HARAKA JAMANI!

    ReplyDelete
  3. kwa maoni ya mwandishi, aluiyaefariki sio muhimu. Hapo unatakiwa ujifunze kitu, akili kichwani mwako.

    ReplyDelete

Top Post Ad