Baada ya Kuachwa na Mbunge na Kulazwa..Yasemekana Wastara Juma Atoroshwa Hospitalini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Taarifa mbaya! Staa wa Bongo Muvi, Wastara Juma ambaye mapema wiki iliyopita alidai kupewa talaka la mumewe, Sadifa Khamis Juma, Mbunge wa Donge, Zanzibar, anadaiwa kutoroshwa hospitalini kisha kupelekwa hoteli ya mafichoni huku akiendelea na matibabu.

Kwa mujibu wa chanzo makini, Wastara aliyekuwa amelazwa kwenye Hospitali ya Misheni ya St. Herry Health Center iliyopo mjini hapa, aliondolewa wodini hapa usiku mnene huku akiwa bado hali yake ya kiafya haijatengamaa tangu alipolazwa mapema wiki iliyopita akisumbuliwa na presha na kisukari na baadaye kupoteza fahamu.

Wikienda lilifika hospitalini hapo Jumamosi iliyopita na kuthibitishiwa kuondolewa kwa msanii huyo na mtu aliyedai kuwa ni babu yake aliyetajwa kwa jina la Abdulaziz Babu.
Kwa mujibu wa mmoja wa wahudumu waliokuwa zamu walioomba hifadhi ya majina, jamaa huyo alidai kuwa Wastara aruhusiwe kwani alihofia usalama wake na kwamba sehemu aliyopanga kumpeleka ni salama zaidi.

Baada ya kunusa ‘ubuyu’ huo hospitalini hapo, Wikienda lilimsaka Wastara kujua mahali alipo na hali yake lakini jitihada hizo ziligonga mwamba kwa kuwa namba yake ya simu haikuwa hewani.

Alipotafutwa mtu huyo anayedai ni babu wa Wastara alifunguka: “Ni kweli nimemuondoa Wastara hapo hospitalini kwa sababu za kiusalama. Yupo hotelini lakini siwezi kukuelekeza ni sehemu gani kwa sababu ukiandika itajulikana na tatizo litakuwa palepale.”

Wastara alikumbwa na hali hiyo ikidaiwa ilitokana na mgogoro wa ndoa yake na Sadifa iliyofungwa hivi karibuni na kushindwa kudumu.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hawezi maisha ya ndoa huyo uolewe Leo kesho ufunguliwe duka nani kasema

    ReplyDelete
  2. Kama kweli anaumwa atarudi hosptalini. Wabongo mna mambo!!

    ReplyDelete
  3. huyu mdada matatizo ya mara kwa mara yameshamharibu akili, sidhani kama ana akili nzuri.

    ReplyDelete
  4. Wanawake wa kitanzania mnachekesha sana, mwanaume ukimpenda si lazima akuahidi vitu, au akufanyie vitu ndio iwe sababu ya kuolewa naye, na sio umpende kwa sababu atakufungulia maduka na unataka afanye hivyo siku 2 baada ya harusi, jamani sijawahi sikia ndio za hivyo mimi. Watu mnatafuta wote na ndio utaiheshimu ndoa yako sio unataka uvikute mwezio amesha tafuta. Nanye wanaume wakitanzanie ukisha ona hivyo kwanini bado unataka ndoa na huyo mtu? ndoa hiyo hawezi dumu maana mwanake hakutaki wewe ila anataka mali zako. Oweni wanawake kutoka marikani wanajua jisi ya kutumza wanaume na ndoa zao nizakudumu.

    ReplyDelete
  5. angetulia kwanza hata hiyo ndoa ilikuwa ghafla sana na kama alimpenda mali ni baadae heshima na penzi kwanza mambo mengine baadae

    ReplyDelete
  6. Wastara anataka mwanamme mwenye pesa tu, baada ya Sajuki kufariki Wastara alienda kwenye mitandao ya kijamii akasema anataka kuolewa na mwanaume mwenye pesa zake sababu anataka kuendesha magari ya kifahari, watu walimtukana ile mbaya, si ajabu Wastara alimroga Sajuki akafariki alivyoona Sajuki hana pesa, maana mpaka leo haijulikan Sajuki alikufa na ugonjwa gani

    ReplyDelete

Top Post Ad