LEO ndio Leo Chadema Kumleta Mrithi Atakaye Vaa Viatu Vya Dr Slaa Kuziba Nafasi ya Katibu Mkuu...

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Katibu mkuu mpya wa Chadema atajulikana leo wakati Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe atakapowasilisha jina la mtu anayempendekeza kushika wadhifa huo.

Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalim alisema jana kuwa jina hilo linatarajiwa kuwasilishwa mbele ya kikao cha Baraza Kuu kinachoanza jijini  Mwanza leo.

"Moshi mweupe kuhusu jina la katibu mkuu mpya utaonekana Jumamosi mchana (leo). Mimi na Naibu Katibu Mkuu mwenzangu John Mnyika tuko tayari kumpokea bosi mpya,” alisema Mwalimu.

Katika kikoa chake na waandishi wa habari kilichohudhuriwa na Mnyika, Kaimu Katibu Mkuu huyo alisema hadi sasa, hakuna yeyote miongoni mwa viongozi na wanachama wa Chadema anayejua kwa hakika nani atarithi mikoba hiyo iliyoachwa na Dk Willibrod Slaa zaidi ya Mbowe.

Alipoulizwa jana, Mbowe hakutaka kuzungumzia suala hilo kwa undani zaidi ya kuahidi kumteua katibu mkuu atakayemudu kubeba dhamana ya kuivusha Chadema salama katika harakati za kushika dola katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu alisema: “Tunaweza kufikia uamuzi kwa maridhiano bila hata wajumbe kulazimika kupiga kura. Hilo naweza kukuhakikishia kwa sababu mimi ndiye mwenyekiti wa kamati ya maridhiano.”

Pamoja na kupitisha jina la katibu mkuu, vikao vikuu vya Chadema ambavyo kwa mara ya kwanza vimefanyika nje ya Dar es Salaam, pia vinatarajiwa kujadili na kuamua mpango mkakati wa kisiasa wa miaka mitano kuanzia sasa hadi 2021, kupitisha bajeti ya chama kwa kipindi hicho na kufanya marekebisho ya katiba, kanuni na miongozo ya mabaraza.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad