TETESI: Clouds FM Kuwatema Baadhi ya Watangazaji...PJ na Gerald Hando Watajwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Habari zinasema kwamba PJ, Abel Onesmo na Gerald Hando watapigwa chini kuanzia mwezi April mwaka huu. Kwa kawaida, Clouds wana utaratibu wa kutoa mikataba mipya kila ifikapo April 1.

Katika zoezi hilo kuna wafanyakazi wapya wanaopewa mikataba na wale wa zamani ambao kituo kinawahitaji "hurenew" mikataba yao.

Imefahamika kwamba PJ , Abel Onesmo na Gerald Hando ambao wote wanatoka kipindi cha Power Breakfast (PB) watapigwa chini mwezi huu au kwa kauli ya mjini ni kwamba "Watatumbuliwa".

Sababu kubwa inayotajwa ya wakongwe hao kupigwa chini ni kushindwa kuendana na taratibu za kampuni hiyo kongwe na kinara katika sekta ya Burudani nchini kwani wanajiona wao wako juu ya watu wote.

Pia inasemekana suala la Rais Magufuli kupiga simu kwenye kipindi cha Clouds 360 limewauma sana kwani walikuwa wanaamini wao ndio kipindi bora zaidi cha asubuhi hivyo Suala la Magufuli kupiga simu 360 limeprove "otherwise".

Inadaiwa kuwa msuguano mkubwa ulianza wakati wa kipindi cha uchaguzi kutokana na kutumika kisiasa na kulipwa na baadhi ya wanasiasa ili watumie Power Breakfast kama jukwaa la kuwasafisha kinyume na maadili ya kazi yao yanayosisitiza "neutrality" katika kutoa habari.

Vilevile habari za kuaminika kutoka ndani ya Clouds zinasema kwamba tayari Clouds Media Group imeajiri vichwa vipya ambavyo kuanzia tarehe 1 vitaanza kupiga kazi.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. clouds imekua kama tbc wana uccm sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. we acha ujinga, CCm gani wakati Cclouds imechukuliwa na Rostam Azizi na wakati huohuo Rostam ni mshirika wa Lowasa? wakina Hando si walikuwa ukawa na mpaka ilifika Hando alizunguka nchi nzima kushawishi watu wapigie ukawa, na hado alikuwa kikabila zaidi kisa mgombea wa ukawa ni mtu kutoka Arusha, fanyeni utafiti kwanza kabla ya kuandika

      Delete
    2. anony 9.59pm heri ungekaa kimyaaaa maana ndio umezidi kudhiirisha hoja ya anony 12.47pm ni kweli ha ha ha ha ah

      Delete

Top Post Ad