Wafanyakazi watatu TANESCO Watiwa Mbaroni Kufuatia Kifo cha Mfanyakazi Mwenzao Aliyenaswa na Umeme Juu ya Nguzo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wafanyakazi watatu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) mkoani Morogoro, wanashikiliwa na Polisi wakihojiwa kutokana na kifo cha mfanyakazi mwenzao, Deo Elias (30), mkazi wa Mazimbu, Manispaa ya Morogoro kwa kunaswa na umeme juu ya nguzo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 5.30 asubuhi maeneo ya Mafiga, wakati Elias akiwa na wafanyakazi wenzake katika eneo la kazi.

Kamanda Matei alisema Elias alipokuwa na wenzake katika eneo hilo wakirekebisha umeme, alinaswa na kufa papo hapo.

Meneja wa Tanesco Mkoa wa Morogoro, Mhandisi John Bandiye akizungumzia tukio hilo ofisini kwake jana, alisema Elias alikuwa katika kazi za kawaida kama fundi na tukio hilo limetokea kwa bahati mbaya.

Mhandisi Bandiye alisema mfanyakazi huyo alikuwa akirekebisha njia ya umeme ya Ngazengwa iliyopo eneo la Mafiga na ilikuwa imezimwa, lakini cha kushangazwa ilikuwa na umeme uliosababisha kifo chake.

“Kwa sasa shirika lina wafanyakzi wa muda wanaosaidiana na mafundi wakuu na hupatiwa mafunzo na wanatambulika, tofauti na maneno yaliyozagaa mitaani kuwa marehemu hakuwa mfanyakazi,” alisema.

Alisema mwili wake umesafirishwa kwenda kwao mkoani Mbeya kwa ajili ya maziko.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. TANESCO ni wazembe sn huko majumbani kila siku watu wanaunguziwa vitu vyao kwa sababu ya kata zima isiyo eleweka ya tanesco,kufa kwa huyo mfanyakazi akiwa kazini nao utakuwa ni uzembe tu wa tanesco ambao imetulazimu wananchi tuone ni kawaida,poleni sn wafiwa

    ReplyDelete

Top Post Ad