Serikali Kuwasilisha Mswada wa Sheria ya Ndoa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Serikali   imejiandaa kuleta Muswada wa Sheria bungeni kutoa haki ya kusoma kwa watoto wote wa kike na kiume wa shule za msingi, sekondari na kutoruhusiwa kuoa au kuolewa.

Aidha, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amesema serikali inaendelea kukamilisha utaratibu wa kupata maoni ya wananchi kuhusu marekebisho ya Sheria ya Ndoa na kutungwa kwa Sheria mpya ya Mirathi na Urithi kuondokana na mkanganyiko uliopo kuhusu sheria hiyo.

Bunge lilielezwa hayo jana mjini Dodoma wakati waziri huyo akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ileje, Janeth Mbene (CCM) aliyehoji ni lini serikali itaanza maandalizi ya kuchukua maoni juu ya kufanya marekebisho sheria ya ndoa ya mwaka 1971.

Akijibu swali hilo, Dk Mwakyembe alisema hatua za awali zimeshaanza kuchukuliwa na wizara hiyo ili kupata maoni ya wananchi juu ya marekebisho ya sheria hiyo ya ndoa ya mwaka 1971 na kutungwa kwa sheria mpya ya mirathi na urithi.

Alisema serikali ina nia ya dhati ya kufanyia marekebisho sheria ya ndoa na kwamba mchakato huo ulisitishwa kwa kuwa Tume ya mabadiliko ya Katiba ilikuwa ikikusanya maoni kuhusu mabadiliko ya katiba , hivyo walidhani wananchi wangetoa pia maoni juu ya sheria hiyo
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kumbe dozi za India zinafanya kazi
    Sumu sumu sumu
    Mbona tusikiiiiiii tena ya sumu
    CCM kwa wanywa dozi India mko wengi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hi dozi na Mimi naitaka jamani ni kada wa CCM

      Delete

Top Post Ad