UVCCM Wamshukia Fredrick Sumaye ..Wamtaka Amwache Rais Magufuli Afanye Kazi Yake..Wadai yeye Alishindwa Alivyokuwa Waziri

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi umesema Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye hana vigezo wala sifa zozote zinazoweza kumfanya awe na uwezo wa kumkosoa Rais Dk John Magufuli katika uendeshaji wa serikali na masuala ya utawala.

Sumaye ametakiwa amuache Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Magufuli ili atimize majukumu yake kwa sababu alipewa dhamana ya kuwa Waziri mkuu lakini hakufikia hata theluthi ya utendaji unaofanyika sasa.

Msimamo huo umetolewa jana na Kaimu katibu mkuu wa uvccm shaka hamdu shaka alipokuwa akizungumza na wanachama wa ccm wa kata mbili za kwandele na mbichi jimbo la Rombo mkoani kilimanjaro.

Shaka alisema anachokifanya Sumaye na baadhi ya wanasiasa muflis wanaojaribu kukosoa utendaji katika utawala wa serikali ya awamu ya tano ni kutaka nao wasikike wakidhani yale walioyafanya wakati wakiwa madarakani wananchi wameyasahau.

Alisema kama yupo waziri mkuu ambaye ameonyesha udhaifu katika utendaji na usimamizi wa serikaki huku akishindwa kumsaidia Rais hakuna atakayempita Sumaye.

Aidha Kaimu huyo alimuonya Sumaye kuacha kumfuatafuata Dk Magufuli katika mikakati yake ya kutumikia nchi na juhudi anazozichukua dhidi ya mafisadi na wabadhirifu wa mali za umma nchini.

Alisema wakati Rais Magufuli akiwa katika dhamira njema na nia ya wazi kuwatumikia wananchi kwa uadilifu, uaminifu na heshima  kina sumaye na wenzake wafumbe midomo yao na waache mara moja kumbughudhi Rais kwa ajili ya kusaka umaarufu wa kisiasa.

Pia shaka aliwataka wananchi wa jimbo la Rombo kujitayarisha ili kumpiga chini mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya chadema Joseph Selasini kwa sabahu ni dhaifu na hatoshi kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo.

"Siku zake za kuitwa mbunge wa Rombo sasa zinahesabika, Selasimi hajui anachokifanya wala hajali shida na matatizo yaliopo katika jimbo lake,lazima adui huyo apigiwe mwaka 2020 "alisisitiza shaka

Akizungumza katika mkutano huo mwenyekiti wa uvccm mkoa wa kilimanjaro Juma Raib Juma aliwakanya wananchi wa kanda ya Kaskazini kuacha mara moja tabia ya kushiriki na kuchagua vyama na wagombea wa nafasi mbali mbali kwa ukabila, ujimbo au nasaba.

Raibu alisema ikiwa wananchi wa kaskazini sasa wanaishi katika Mikao yote ya Tanania, si jambo la maana wao wakahesabiwa kama ni wabaguzi kwa misingi ya asili au ujamaa.

"Tunachotaka kukisafanya baadhi ya wananchi wa Mikao ya Kaskazini ni kumuasi baba wa Taifa marehemu Mwalimu julius Nyerere, hakutuacha tukiwa tumegawanyika , tumeishi miaka yote hatukuongozwa kwa ukabila au udini, chadema acheni kwasabahu hilo ni balaa au janga katika jamii "alisema Raib.

Jumla ya wanachama wapya 103  walijiunga na chama cha mapinduzi pia shaka alipata nafasi ya kuangalia mechi ya soka kati ya timu za kata za makiidi na mahare wilaya ya Rombo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jifunzeni makosa wanayokoselewa viongozi wenu wa CCM
    Hata papa anakwenda na wakati sembuse CCM

    ReplyDelete
  2. Huyo Sumaye alikuwa kwanza fisadi tu nae, hana lolote sijui wamesha firisika kimali mpaka mawazo, muda wake ushapita, aende na alama za nyakati asibaki kubwabwajabwabwaja hapa, mwisho wa siku ataonekana mjinga, akae kimya tu atumie pension yake, anaogopa kusahaulika katika masikio ya watanzania? Ndivyo maisha yalivyo

    ReplyDelete
  3. Kwa nini kisomo cha Watanzania wengi ni duni. Mtu unatetea chama na raisi hata akifanya makosa. Magufuli ni Raisi wa nchi na akumbushwe hivi. Yeye si Raisi wa CCM. na vijana wote wa CCM mnashindwa kujua hili. Utamwachaje Raisi afanye apendavyo wakati kuna sheria za nchi. Vijana kundi nzima mnashindwa kutenganisa chama na serikali. Sasa wote wanaccm kama hamuoni hili, mbona Taifa limeshuka sana kielimu. Sifa moja ya uraisi ni kuwa katikai . si kuelekea kichama. Na kwa nini Watanzania wengi wavivu kujisomesha ili wajue sheria za nchi. Tunahitaji elimu kwa vijana kwa sasa. Au la taifa litazorota, halina uhuru, tunarudia unyanyasaji. Katiba ya wananchi inahitajika sasa ili Sheria za nchi zifuatwe na viongozi wa ngazi zote nchini. Huwezi kumkubalia Ndugu Magufuli atumbue watu kwa kuchagua apendavyo huku akiwaacha majipu makuu ya Serikali yaliyoifikisha nchi hii hapa tulipo. Ni Raisi Kikwete na mwenyekiti wa CCM ndiye aliyeipeleka Nchi hapa tulipo. Ukweli unauma. Magufuli Hangekuwa na haja ya kutumbua majipu kama Raisi Kikwete angefuata sheria za nchi kwa miaka kumi iliyopita. Mnatumbua samaki wahusika wakuu wakijisafisha kuleta idadi za mali zao na mnazificha kwa nini. Raisi wa Marekani anaweka mshahara hadharani, koni anayolipa hadharani, pesa aliyopata kwa kuandika vitabu hadharani, Zawadi alizopata Mkewe zinapelekwa kwenye museum ya Taifa. Nyinyi bado mnadanganya watu kama hawajui kujisomea, kama hawana akili, kama mizoga. Tanzania acheni kuwahadaa wananchi. Tumbueni watu wa Escrow, Waliotoa vibali kuwindia kwa wafalme wakiarabu, marekani na mabilionea wengine. Huu ni wizi wa mali za umma. Mali za Watanzania, Wagonjwa, Wazee, Watoto, Wanafunzi. Kama Raisi magufuli ni mkristo kweli, akumbuke amepewa mamlaka ya kuwatetea hawa na si kula na mapadre wala maaskofu. Inabidi ale na Watoto Yatima, Wagonjwa, Wasiojiweza, Wazee, Vipofu. Unamkumbuka Sokoine Sokoine hakuwa hivi, msijipe majina na kujilinganisha na viongozi waliopita kwa kuwahadaa wananchi. Ardhi zilizotolewa bure kwa Wazungu wenye utajiri kwao kupindukia na hawashibi hata. Wanawaleteeni vijisenti mnawapa Ardhi, madini, mikataba bure. Na wengi mawaziri wamehongwa na wanaaccount nje. Hizi ni mali za maskini Watanzania mnaowaibia kutokana na vyeo na ujanja kupitia elimu za wasiwasi bila kuwa na majivuno kama mwafrika mwenye heshima na ustaarabu.Nawaombeni WanaCCM wote toka ngazi za juu, mktaka maendeleo, Toa uhuru wa mawazo, na muwafungulie kesi hawa wote walioifikisha Tanzania njia panda kwa miaka kumi. Si kushangilia vijisamaki vidogo vinavyoshikwa na madingi wamelalia mabillioni ya wizi vitandani,.

    ReplyDelete

Top Post Ad