Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) Profesa Tunus Mgaya Aliyesimamishwa Kazi na Waziri wa Elimu Afunguka Mambo Mazito

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

ALIYEKUWA Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Profesa Tunus Mgaya amesema amesikitishwa na taarifa zilizoandikwa katika vyombo vya habari za kukosoa maamuzi ya serikali ya kuwasimamisha kazi kuwa hayakuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa.

Mgaya ambaye hakuwa tayari kueleza kama taratibu za kusimamishwa kwao zilifuata utaratibu au la, amewataka waandishi wa habari kuwa na vyanzo vya uhakika katika habari zao.

“Mimi nikiwa miongoni mwa watendaji waliopumzishwa kazi, napenda kueleza kuwa sihusiki na taarifa hizo, suala hili limeshapita na kutolewa uamuzi na serikali na tuiache Tume iendelee kufanya kazi,” alisema Profesa Mgaya alipozungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kukabidhi ofisi.

Aidha, Profesa Mgaya aliweka wazi kuwa, anaunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika kuhakikisha kuwa watanzania wengi zaidi wanapata elimu ya msingi bure na kutolewa kwa elimu inayokidhi viwango stahiki kitaifa na kimataifa na kusema jambo hilo ni jema na linapaswa kuungwa mkono kwa nguvu zote.

Katika hatua nyingine, alimtaka Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na Ufundi , Profesa Joyce Ndalichako kuendeleza jitihada za kuinua ubora wa elimu katika ngazi zote ili kuwa na taifa lenye watu walioelimika vizuri na lenye mchango mkubwa katika kuendeleza taifa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kweli wewe ni profesa maana unayoongea yanalingana na elimu uliyonayo.Haijalishi ni boss au sio,Kusimamishwa kazi ndio njia sahihi ya kupisha uchunguzi na ikibainika huna kosa unarudishwa kazini na stahiki zako unapewa,tatizo liko wapi watanzania wenzangu?

    ReplyDelete

Top Post Ad