Mtoto wa Chacha Wangwe Abadili Msimamo Mahakamani Kwenye Kesi ya Kuchapisha Taarifa za Uongo Mtandaoni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mtoto wa Chacha Wangwe Akiwa Mikononi Mwa Polis
Mtoto wa aliyekuwa mwanasiasa machachari na Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, amebadili msimamo mahakamani katika kesi ya kuchapisha taarifa za uongo kupitia mtandao wa kijamii, kuwa Zanzibar inakandamizwa na Tanzania Bara na kwamba ni koloni lake.

Mtoto huyo, Bob Chacha Wangwe (24), ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alibadili msimamo jana aliposomewa shtaka hilo kwa mara ya pili, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wangwe alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Mei 11, na alisomewa shtaka linalomkabili na alikiri kutenda kosa hilo.

Mshtakiwa anapokiri kosa, kwa kawaida Mahakama inaweza kumtia hatiani na kumpa adhabu kwa mujibu wa sheria, kulingana na kosa siku hiyo hiyo au siku nyingine yoyote.

Baada ya kusomewa shtaka na kukiri, Hakimu Mkazi Mkuu, Waria lwande Lema, aliamuru mshtakiwa huyo apelekwe rumande hadi jana, Mei 17, kwa kuwa hakimu aliyepangwa kusikiliza kesi hiyo hakuwapo.

Hata hivyo, jana mshtakiwa huyo alipopandishwa kizimbani na kusomewa shtaka hilo, ili kusomewa maelezo ya awali kabla ya Mahakama kumtia hatiani na kumhukumu, tofauti na siku ya kwanza, alikana kutenda kosa hilo.

Kutoka na mshtakiwa huyo kukana kosa, Wakili wa Serikali, Salim Msemo, aliieleza Mahakama kuwa upelelezi bado haujakamilika, hivyo aliiomba ipange tarehe nyingine ya kutajwa kwa kesi hiyo.

Wakili wa mshtakiwa huyo Peter Kibatala aliiomba Mahakama impe dhamana kwa kuwa shtaka linalomkabili linadhaminika, maombi ambayo yalikubaliwa na aliachiwa kwa dhamana na kesi iliahirishwa hadi Juni 15.

Wangwe ambaye baba yake kwa sasa ni marehemu, anadaiwa Machi 15, jijini Dar es Salaam, alisambaza taarifa za uongo kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Alisambaza taarifa za uwongo au Alisambaza taarifa za kweli?manake ukisema ukweli basi serikali ya dikteta magufuli itakushughulikia,na ndio yaliyomkuta Wangwe

    ReplyDelete

Top Post Ad