Nape Nnauye Ashindwa Kuhutubia Kwenye Tamasha la Muziki Jijini Mwanza Kutokana na Zomeazomea Ya Wananchi Wanaotaka Bunge Lionyeshwe Live

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mzimu wa kuzuia shughuli za Bunge kuonyeshwa moja kwa moja na vituo vya televisheni uliopachikwa jina la ‘Bunge Live’, umeendelea kumwandama Waziri wa Habari, Nape Nnauye baada ya juzi kupokewa kwa kelele kiasi cha kushindwa kuhutubia wapenzi wa muziki jijini Mwanza.

Nape alitangaza uamuzi wa kusitisha kurusha moja kwa moja baadhi ya shughuli za Bunge, akisema Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) linashindwa kumudu gharama, lakini wabunge, hasa kutoka vyama vya upinzani wamepinga hatua hiyo wakisema inawanyima wananchi haki yao ya kikatiba ya kupata habari kuhusu chombo chao cha kutunga sheria.

Lakini Serikali imeshikilia msimamo wake, ikitoa sababu tofauti na kwenda mbali zaidi kuzuia vituo binafsi vya televisheni kurusha matangazo, huku TBC1 ikirusha kipindi cha maswali na majibu pekee ikielezwa kuwa huo ni uamuzi uliopitishwa katika Bunge la 10.

Juzi, Nape aliyekuwa mgeni rasmi katika tamasha la Jembeka Festival lililofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, alipokewa na kelele za maneno “Bunge Live” wakati akikaribishwa kuhutubia mamia ya wapenzi wa burudani waliohudhuria tamasha hilo, ambalo lilijumuisha wasanii nyota kama Shaffer Chimere Smith a.k.a Ne-Yo kutoka Marekani na Diamond Platnum.

Baada ya mkurugenzi wa kampuni ya Jembe ni Jembe, Sebastian Ndege kumkaribisha waziri huyo kuzungumza na wananchi hao, Nape alisimama lakini akapokewa kwa kelele.

“Bunge live, Bunge live, Bunge live,” walipiga kelele mashabiki waliohudhuria tamasha hilo.

Kelele za “Bunge Live” zilisababisha Waziri Nape kushindwa kuhutubia na kulazimika kuketi chini na Mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula alisimama kujaribu kuokoa jahazi, lakini naye akakumbana na kimbunga cha sauti za wananchi walioamua kulitaja jina la mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Ezekia Wenje.

“Wenje, Wenje, Wenje,” wananchi hao waliimba kwa sauti wakati Mabula akijaribu kuwatuliza ili Nape ahutubie.

Akizungumzia tukio hilo, Nape alisema wananchi waliompigia kelele za “Bunge Live” walisukumwa na masuala ya kisiasa, ndiyo maana aliepuka kuendelea kuzungumza ili kutochafua hali ya hewa uwanjani.

“Pale uwanjani tulikwenda kwa ajili ya burudani, sasa baada ya kuona wananchi wanaanza kuleta masuala ya kisiasa nikaona ni busara kuacha kuhutubia. kuepusha shari,” alisema Nape.

Pamoja na Nape, tamasha hilo pia lilihudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano), January Makamba, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na Mabula.

Ukiachilia mbali dosari hizo, tamasha hilo lilikonga nyoyo za wapenzi wa sanaa ya muziki waliokesha uwanjani hapo hadi saa 11:00 alfajiri wakiburudishwa na wasanii nguli.

Wasanii wengine waliopata nafasi ya kutumbuiza ni Juma Nature, Ney wa Mitego, Ruby na Fid Q.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Haya ni madogo na kuto kuelewa hali halisi ya wabunge wetu na mshinikizo wao wa kisiasa.. Sisi wananchi tulio wengi baada ya kuona wabunge na timbwili zao ndani ya bunge na ukosefu wa nidhamu waliudhihirisha na kutojali maadili yaliyopo ndani ya Bunge imewafanya kuwa wao tunaowategemea na ambao tumewaanini katika chombo cha kutunga sheria wamekuwa ndiyo wa mwanzo kuvunja sheria.. Hii ya kutojuwa laivu tunaiunga mkono na Nape wala asilaumiwe au kufikiriwa kwamba yeye ndiyo mtendaji mkuu wa hili... Nape tumempa wadhifa na Anawajibika katika awamu yetu ya TANo chini ya Baba JPJM na Mh Kassim Majaliwa... Nia njema wanayo .. Uwezo wanao na ni juu yetu sisi wanachi kuwaunga mkono na kuwasaidia katika utendaji wao ili kufanikisha malego waliyo nayo katika kututumikia sisi wanachi na Nchi... Chonde chonde yasiyo na umuhima msifafanye kuwa ni muhimu maana yake yatakula wakati ambao tunauhitaji katika gurudumu la kuleta MAENDELEO ya nchi yetu na Hawa WACHAPAKAZI WETU TUSIWACHOSHE HARAKA>> NIA ZAO NA DHAMIRA ZAO NI NJEMA KWA TAIFA LETU.. TUWAJIBIKE INAVYOSTAHILI... MUNGU AWABARIKI NA KUWAPA UMURI TAWILE.. ILI TUONE MATUNDA YETU KUTOKANA NA UONGOZI WAO.. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE... NAPE ENDELEA NA UAMUZI TUMEKUPA SISI HATUTAKI LAIVU WALA USIPOTEZE HOJA ZA KUWAJIBU HAO WATAKAO LAIVU (ISSUE IS CLOSED CHAPTER TUANGALIE YA MBELE)

    ReplyDelete
  2. Haya ni madogo na kuto kuelewa hali halisi ya wabunge wetu na mshinikizo wao wa kisiasa.. Sisi wananchi tulio wengi baada ya kuona wabunge na timbwili zao ndani ya bunge na ukosefu wa nidhamu waliudhihirisha na kutojali maadili yaliyopo ndani ya Bunge imewafanya kuwa wao tunaowategemea na ambao tumewaanini katika chombo cha kutunga sheria wamekuwa ndiyo wa mwanzo kuvunja sheria.. Hii ya kutojuwa laivu tunaiunga mkono na Nape wala asilaumiwe au kufikiriwa kwamba yeye ndiyo mtendaji mkuu wa hili... Nape tumempa wadhifa na Anawajibika katika awamu yetu ya TANo chini ya Baba JPJM na Mh Kassim Majaliwa... Nia njema wanayo .. Uwezo wanao na ni juu yetu sisi wanachi kuwaunga mkono na kuwasaidia katika utendaji wao ili kufanikisha malego waliyo nayo katika kututumikia sisi wanachi na Nchi... Chonde chonde yasiyo na umuhima msifafanye kuwa ni muhimu maana yake yatakula wakati ambao tunauhitaji katika gurudumu la kuleta MAENDELEO ya nchi yetu na Hawa WACHAPAKAZI WETU TUSIWACHOSHE HARAKA>> NIA ZAO NA DHAMIRA ZAO NI NJEMA KWA TAIFA LETU.. TUWAJIBIKE INAVYOSTAHILI... MUNGU AWABARIKI NA KUWAPA UMURI TAWILE.. ILI TUONE MATUNDA YETU KUTOKANA NA UONGOZI WAO.. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE... NAPE ENDELEA NA UAMUZI TUMEKUPA SISI HATUTAKI LAIVU WALA USIPOTEZE HOJA ZA KUWAJIBU HAO WATAKAO LAIVU (ISSUE IS CLOSED CHAPTER TUANGALIE YA MBELE)

    ReplyDelete
  3. Haya ni madogo na kuto kuelewa hali halisi ya wabunge wetu na mshinikizo wao wa kisiasa.. Sisi wananchi tulio wengi baada ya kuona wabunge na timbwili zao ndani ya bunge na ukosefu wa nidhamu waliudhihirisha na kutojali maadili yaliyopo ndani ya Bunge imewafanya kuwa wao tunaowategemea na ambao tumewaanini katika chombo cha kutunga sheria wamekuwa ndiyo wa mwanzo kuvunja sheria.. Hii ya kutojuwa laivu tunaiunga mkono na Nape wala asilaumiwe au kufikiriwa kwamba yeye ndiyo mtendaji mkuu wa hili... Nape tumempa wadhifa na Anawajibika katika awamu yetu ya TANo chini ya Baba JPJM na Mh Kassim Majaliwa... Nia njema wanayo .. Uwezo wanao na ni juu yetu sisi wanachi kuwaunga mkono na kuwasaidia katika utendaji wao ili kufanikisha malego waliyo nayo katika kututumikia sisi wanachi na Nchi... Chonde chonde yasiyo na umuhima msifafanye kuwa ni muhimu maana yake yatakula wakati ambao tunauhitaji katika gurudumu la kuleta MAENDELEO ya nchi yetu na Hawa WACHAPAKAZI WETU TUSIWACHOSHE HARAKA>> NIA ZAO NA DHAMIRA ZAO NI NJEMA KWA TAIFA LETU.. TUWAJIBIKE INAVYOSTAHILI... MUNGU AWABARIKI NA KUWAPA UMURI TAWILE.. ILI TUONE MATUNDA YETU KUTOKANA NA UONGOZI WAO.. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE... NAPE ENDELEA NA UAMUZI TUMEKUPA SISI HATUTAKI LAIVU WALA USIPOTEZE HOJA ZA KUWAJIBU HAO WATAKAO LAIVU (ISSUE IS CLOSED CHAPTER TUANGALIE YA MBELE)

    ReplyDelete
  4. Ni watu kama nyinyi mnaopotosha nchi na kudhani watsnzania bado hawajafunguka macho bado ndio hawa wamechaguliwa na watu, watu wanajua sheria safi ni nyinyi na viongozi wengi wa Serikali hawajui na hawatambui umuhimu wa uhuru wa watu wa nchi.ni hawa watu ndio wananaounda serikali.unatambua ya kwamba watanzania ndio serikali, na hawa viongozi ni wawakilishi tu.nhi itakuwa huru na itaendlea na kupata ushirikiano safi ikiwa viongozi wetu watajua watu ndio wenye neno la mwnwisho na wasikilizwe badala ya kulazimisha mambo kama wakoloni zamani au dini.wakoloni walilazimisha sababu kichwani mwao uswa haukuwepo, heshima haikuwepo, ni utii tu walitegemea wala kuuliza swali.hii iliwasaidia wao kuburuza watu na kuwalazimisha kwa nguvu ili wawatimizie maslahi yao. Leo tumejikomboa kielimu, kifikra, tunajitawala. Lakini viongozi wetu hawa ingawa ni wasomi lakini bado wamejiweka watawala. Ni kwa kuuficha udhaifu wao kwani wengi wabunge uwezo wao mdogo.na wengi hoa viongozi wanaficha udhaifu wao.hawajui watu waliowachagua wanataka kuwafuata wazi ili wajua kitu gani kinaebdelea na ili kutoa bifu ya kisiasa.hapa Nape umejionea mwenyewe watu wanadai haki zao.uwasikilize na ujue hii ni haki ya watanzania wote. Si kazi yenu kuwadharalisha kuwadharau leo wamepata mwanya wa kukudharalisha hadharani kama ulivyowadharalisha ukiwa bungeni bila aibu.hii uionje kwani wameionja wao kwanza. Na wamejua mmempachika huyu bwana kinguvu.wanajua kwani wao ndio waliopiga kura na kumchagua mtu wanayempenda awaongoze ni nyinyi ccm mmempachika huyu pia. Kuna uhuru wa kupiga kura ambao nyinyi wachache bado hamuuheshimu.na watu wa mwamza nawasifu walivyofanya kutetea uhuru wao hadharani. Na bado ..kama mnavyowaomba ushirikiano nanyi, mjua hamwezi kuupata ushirikiano safi. Laini, wakijuamnawawanyima uhuru wao.wataendelea zomea.bungeni pia mnalazimisha na kuingiza polisi kamatakamata, je mtainguza polisi wakamate uwanja mzima.wengi wape, hata kwa nguvu watachukua.na ningependa watanzania waache woga pale wanaponyimwa haki na kuonewa. Waungane pamoja bila kjali itikadi ili wapate haki zao.
    Mwisho namalizia, ingawa namsifu Magufuli naomba awatendee haki watanzania, weka katiba ili turudishe heshima na sheria nchini. Tumbua wakuu wa nchi walioruhusu nchi kufikia hapa tulipo.watu wote wanawajua ni nani. Umesema hutamwacha mtu.na hutawakumbatia.ni hawa walishindwa kusimamia nchi, kulinda watu na mali zao, arddhi, madini, maji,elimu, mahospitali,mashule na nyumba za mali ya umma. Walikaa kimya na kuangalia nchi inaliwa. Kwa jambo hili pia wao ni wahujumu.achenikuficiana madhambi, kulindanana, kama ulivyosema cheo ni dhamana wameshindwa kutumia vyeo vyao.. safi.
    Naomba Mungu akulinde tenda haki bila woga. Napale unapokuwa dhaifu wasikilize watanzania na uwajali na kuwapa haki zao.hao wanaotetea hapo juu ni kati ya wale wanaolindana na wanaufinyu kifikra. Inabidi waone mapungufu na mazuri na mapungufu yasahihishe ili nchi iendelee.

    ReplyDelete
  5. Wewe uliyeandika huo ujinga hapo juu ni Mp.uuzi sana kama maneno yako na yafaa kupuuzwa kama ulivyo Mp.uuzi.kitu kizuri ni kwamba wananchi walishasema walichotaka kusema na ujumbe umefika mahala husika salama ukiwa wa moto kama ulivyopikwa.hongereni wakazi wa mwanza kwa kujitambua na kukataa uzezeta

    ReplyDelete
  6. #bungelive tunataka #bungelive

    ReplyDelete
  7. Bunge laivu not bungelaivu.... Tunacho taka ni maamuzi ya maendeleo na siyo SURA za wabunge... Tumechoka vitimbi vyao... Hatutaki ... Jamani hatutaki..Kuona utumbo na manyaunyau yao.. INATOSHA.... Mpaka watakapo jiheshimu.

    ReplyDelete

Top Post Ad