Wema aweka wazi kuhusu mimba, alivyojigundua mpaka ilivyoharibika ‘nikaona donge la damu likidondoka’

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mashabiki wa malkia wa filamu, Wema Sepetu pamoja na wadau wa burudani walikuwa bado wanamaswali mengi kuhusu mimba ya Wema Sepetu huku wengine wakihisi labda zilikuwa ni kiki, lakini Jumamosi hii staa huyo amefunguka kinagaubaga kuhusu sakata hilo.

Akizungumza na gazeti la Mwanaspoti, Wema alikiri kwamba ni kweli alikuwa ni mjamzito.

“Nilikuwa na ujamzito kweli,” alisema Wema. “Mwezi wa 12 mwaka jana, nilikuwa najihisi kuongezeka uzito, hivyo nikaenda kwa daktari kwa lengo la kusafisha kizazi. Nilipofika kwa dokta nilimwambia hata hivyo nimemisi period, akaniambia ya Mungu mengi pengine nime-concive, nilimkatalia katakata.”

Wema anaendelea kwamba daktari alimshauri akanunue kipimo cha ujauzito ajipime haja ndogo atakapoamka asubuhi na asile kitu chochote kwa ajili ya zoezi la kusafisha kizazi.

“Nilipokuwa narudi nyumbani nilipitia dukani na kununua kipimo hicho na asubuhi nikafanya hivyo, nilishtuka sana, nilikuwa kama nimewehuka nilipoona mistari miwili katika kipimo, siku zote nilizoea kuona mstari mmoja. Nikawauliza rafiki zangu nikiwa katika hali ya furaha baadaye nikampigia daktari nikamwambia nimepima lakini sielewi ninachokiona maana kuna mistari miwili, aliniambia niende na kipimo hicho na akanihakikishia kwamba nilikuwa na ujauzito, sikutaka kumwamini, nikamtaka anipime, hapo ndipo nilipothibitisha, nilisema sasa watanikoma,” anasema.

Baada ya fuhara ya muda mchache akisubiria kupata mtoto, aliona dalili mbaya katika mwili wake.

“Siku ambayo sipendi kuikumbuka ni ile niliyokwenda msalani kwa ajili ya kujisaidia haja ndogo kisha nikaona donge la damu likidondoka, nilichanganyikiwa kwa kuwa daktari aliniambia sikutakiwa kuona damu. Nilipompigia mama yangu naye alinilaumu sana badala ya kunipa pole aliniambia, ‘Wema nilikuambia mimba haitangazwi!, unaona sasa kilichotokea, niliyajua madhara ya kufanya hivyo!”

Wema alisema alikwenda kwa daktari akiwa na Idris kuthibitisha ni kweli ujauzito ulikuwa umetoka na ulikuwa na wiki 13.

Wema anasema, daktari alimwambia ndugu yake mwingine aliyeambatana naye kwamba ujauzito huo ulikuwa ni wa watoto wawili, yaani pacha.

Source: Mwanaspoti
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Acha uongo Wema. Mimba ya wiki 13 haifanani na lile tumbo lako feki la matambara.

    ReplyDelete
  2. Wema yaani kama mtoto mjinga. Details zote za nini? Sema nilikuwa mjamzito bahati mbaya mimba ilitoka ...

    ReplyDelete
  3. Wema acha uongo haukuwa na mimba vipi utadanganya mpaka lini kila mtu anajua ilikuwa mimba feki

    ReplyDelete
  4. pole wema!!!

    ReplyDelete
  5. Halafu haoni haya kusema eti ile mimba feki ilikuwa mapacha. Hajawahi kuwa na utra sound. Kaona damu ambayo ni ya period. Anaita mimba imetoka. Khaa. Ndio maana Mungu kamlani na kumpa ugumba. Kaamua kumgamda yule mwanae wa kufikia aolewe kutoa nuksi. Malaya mbovu kama lile kubwa jinga analoliita mama. Mfyuu

    ReplyDelete
  6. Huyu dada ana matatizo anapenda sifa wakianza kumtukana anaanza kulia.

    ReplyDelete

Top Post Ad