Thomas Ulimwenge Ataja Kilichoipa Ushindi TP Mazembe Jana Kwa Yanga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Thomas Ulimwengu
Mtanzania aliyebaki kwenye kikosi cha TP Mazembe Thomas Ulimwengu alikuwa ni sehemu ya wachezaji waliocheza kwenye mchezo dhidi ya Yanga na kuisaidia timu yake kupata ushindi wa bao 1-0 na kujiweka pazuri kwenye Kundi A baada ya kuvuna point sita katika michezo miwili waliyoshuka dimbani.

Bada ya game kumalizika, ulimwengu amesema siri ya ushindi ya Mazembe inatokana na muunganiko wa professional players wengi wenye uzoefu kwenye timu yao.

“Nilisema mwanzoni kwamba tunakuja kuchukua ushindi, Yanga ni timu nzuri kama mlivyoona wamecheza vizuri lakini kama professional players wengi wenye uzoefu tumeonesha uwezo wa kupata ushindi kwenye mechi ya leo”, amesema Ulimwengu ambaye awali alisema yeye amekuja kucheza nyumani na siyo ugenini.

“Nawapa changamoto wachezaji wa Tanzania watoke wengi tupate professionals wengi ili tuweze kuisaidia timu yetu ya taifa.”

“Yanga bado wananafasi, mechi bado ni nyingi wakishinda wanaweza wakapita kwenye kundi na kwenda hatua inayofuata”, alimaza nyota huyo wa Stars ambaye kocha wake pia alimwagia sifa lukuki kutokana na kiwango alichokionesha kwenye mchezo wa leo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad