Wabunge wa CCM Wavutana Kuhusu Kupatanishwa Kwa Naibu Spika Tulia na UKAWA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mbunge wa Kasulu Mjini (CCM), Daniel Nsanzugwako amesema bado anaamini katika upatanisho kati ya wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson ili kumaliza tofauti zao.

Mwenyekiti mwenza wa Ukawa James Mbatia amesema wameamua hawatasalimiana na wabunge wa CCM, wala kushirikiana nao kwenye shughuli mbalimbali.

Hata hivyo, Nsanzugwako alisema jana kuwa hawezi kufahamu kama mawazo yake aliyowahi kuyatoa bungeni wakati akichangia hotuba ya bajeti kuu mwaka 2016/17 yamefanyiwa kazi.

Bado ninaamini katika kukaa pamoja na kujadiliana, miye ni muumini wa reconciliation (upatanishi) na Bunge ni taasisi siyo mtu binafsi hatuwezi kukaa sisi wanaCCM pekee yetu,” alisema Nsanzugwako.

Akichangia katika hotuba ya bajeti wiki iliyopita, Nsanzugwako alimshauri Dk Ackson kuwasamehe wabunge wa kambi ya upinzani na wakae meza moja kujadiliana na kuondoa tofauti zao.

Nsanzugwako alihoji faida wanayoipata wabunge wa CCM kwa wabunge wa Kambi ya Upinzani kususa vikao vinavyoendeshwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.

Kauli hiyo ilionekana kutowafurahisha wabunge wa CCM na Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde alimpatia taarifa Nsanzugwako kuwa hakuna mbunge wa upinzani aliyefukuzwa na Naibu Spika na kwamba kumuomba Dk Tulia awasamehe ni kuondoa ukweli kwamba wabunge wameadhibiwa na Bunge zima na siyo Naibu Spika.

Dk Tulia alisema hakuna mbunge aliyefukuzwa ila wabunge hao wameamua kuondoka kwa utashi wao wenyewe.

Alisema kanuni ya tano ya Bunge imetoa mwongozo wa jinsi ya kuwasilisha malalamiko ya wabunge wanapokuwa na jambo na kiti.

Alisema tayari wabunge wa kambi hiyo wamewasilisha malalamiko yao jambo ambalo ni haki yao kimsingi . Alisema katika Bunge lililopita wapinzani waliwahi kutumia kanuni hiyo kuwasilisha malalamiko yao dhidi ya kiti, lakini hawakususia vikao vya Bunge.

"Napenda kumfahamisha mheshimiwa mbunge kuwa hakuna mtu waliyemuudhi wala wanaohitaji kuomba msamaha. Wao wametoka kwa utashi wao,”alisema.

Katibu wa wabunge wa CCM, Jasson Rweikiza, alisema hizo ni fujo tu za wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani na kwamba hakuna kitu wanachopoteza kwa wao kutoka nje ya Bunge.

Alisema kanuni zinajieleza jinsi ya kufanya iwapo kuna mbunge hakubaliani na kiti cha Spika kwa kupeleka malalamiko yake katika Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

 “Sisi tutafanyaje sasa kama watu wameamua kufanya fujo, sisi tumeendelea na shughuli za Bunge kwa kujadili kwa kina hotuba zote na kutoa mapendekezo yetu,” alisema.

 Alisema kutoka kwa wapinzani hakuna jambo lilipungua kwani mambo yote yamekwenda sawa na sasa watajadili Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2016 ambayo tayari wabunge wa CCM wamepeleka majedwali ya marekebisho.

Sisi hatuwezi kumlazimisha mtu atupende. Kutoshiriki kwao vikao kunaondoa maana nzima ya kuwa wabunge. Safari ijayo wananchi wasiwachague hawa wahuni, wawachague wabunge wanaotokana na CCM,” alisema.

Hata hivyo, katika kikao cha wabunge wa CCM walichofanya katika ukumbi wa Pius Msekwa na kuongozwa na Mwenyekiti wao Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jana wabunge walijadili mambo mawili.

Miongoni mwa mambo hayo ni hofu waliyonao baada ya wabunge wa upinzani kukataa kusalimiana nao na kushirikiana nao kwenye shughuli mbalimbali na kuelezwa kwanini muswaada wa Sheria ya Fedha haujaenda bungeni hadi sasa.

Wabunge hao walielezea hofu waliyonayo juu ya kufanyiwa vitendo vibaya na wabunge wa kambi ya upinzani. Majaliwa aliwaondoa hofu wabunge hao na kwamba hawana haja ya kuwa na hofu kwa sababu nchi iko salama.

Hata hivyo, aliwataka kuwa wavumilivu na kuendelea kushirikiana nao.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huyu mbunge Nsazugwako ana busara sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sana na anaelewa maana ya upinzani Bungeni coz kuna mambo CCM hawawezi kukosoa wakiwaogopa watawala wao.

      Delete

Top Post Ad