Wanasayansi: Mugabe ana Vinasaba vya Kuishi Milele

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

WANASAYANSI maarufu kutoka Taasisi moja kubwa ya Sayansi nchini Uingereza wametoa ripoti ya utafiti walioufanya ikithibitisha kwamba, Rais wa Zimbabwe, Komrade Robert Mugabe amegundulika kuwa na vinasaba (genes) ambavyo vitamfanya aishi milele (asife).



Robert Mugabemiaka ya 1980.


Utafiti huo wa siri unaongozwa na Daktari Irvin Koch umegharimu mabilioni ya fedha na kugundua pia kwamba Bob Robert mwenye miaka 92 sasa haweki dawa kichwani (SUPER BLACK) wala hajawahi kukata nywele zake licha ya kutojihangaisha na kula vyakula vya mimea (veggies) ama kwenda gym kufanya mazoezi.


Katika tafiti hiyo, Wanasayansi hao walichukua sampuli mbalimbali kutoka kwa Bob ikiwemo damu yake, nguo zake, miswaki aliyokuwa akitumia, na hata chanuo kwa miongo kadhaa na kugundua kuwa hakuna hata chembe ya umauti kwa Mugabe.

Baadhi ya watu wameanza kuamini kuamini tafiti hizo baada ya kugundua kutoka kwenye picha za Mugabe akiendelea kupeta katika muonekano huohuo huku akiwa mwenye siha ya haja kwa miaka mingi sasa.


Mpinzani wake mkuu kwenye siasa za Zimbabwe ambaye ni Kongozi wa Chama cha MDC, Morgan Tsvangirai (ama kwa kuguswa kwamba ausahau uraisi) amejibu kwa kejeli kwamba ‘Mugabe ni makusanyo ya nyama na mifupa kama hayawani wengine wote’ na kwamba kila nafsi itaonja mauti (Kulu ‘nafsi dhaaikatul ‘maut).

Inasemekana kwamba utafiti huo unaendelea mpaka mwaka 2018 ndipo utakamilika.

Source: Newssa/Mzansi Satire


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nyie pamoja na TB Joshua mnakufuru sana kana kwamba hamtakutana na muumba,amini nawaambia ipo siku mtamkuta mungu wa kweli na kwake mtajuta!

    ReplyDelete
  2. ingawa Mugabe ana miaka 92 na yupo mzima mbona ameanguka mara nyingi tena live, kuanguka huko kunaonyesha kuwa moyo wake ni wa kizee kuwa hayupo sawa kuwa moyo umechoka, mbona wapo watu ambao wanaishi mpaka miaka mia na kitu, babu yangu mimi yupo bongo na leo hii ana miaka 97 lakini ameumwa sana hizi siku za karibuni

    ReplyDelete
  3. sio muda mrefu katika social media walionyesha jinsi mke wake na Mugabe akimbagua kisa ni mzee kuwa ana tabu ya kula chakula mwenyewe, walionyesha picha wakati mugape akila chakula na mke wake alikuwa akimuangalia kwa hasira sana yeye mwenyewe Mugabe amelalamika miaka mingi kuwa mke wake ambaye ni mdogo sana kwake amekuwa akimbagua kisa ni uzee

    ReplyDelete
  4. nyerere alisema anauhakika wa kumuona rais wa awamu nyengine alifika? naona hana mda atakufa kwa hii kufru yao. ALLAH NI MKUBWA BWANA

    ReplyDelete
  5. hao watafiti wasitudanganye hawawezi kuingilia uumbaji wa mungu

    ReplyDelete

Top Post Ad