CHADEMA Watangaza Kuanza Operesheni ''Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (UKUTA)''

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Leo Kamati Kuu ya CHADEMA imefanya kikao chake katika Hoteli ya Bahari Beach Ledger Plaza.

Mojawapo ya Maazimio ya Kikao hicho ni kuundwa kwa kile walichokiita Umoja Wa Kupinga Udikteta Tanzania(UKUTA). Tuweke Kumbukumbu sahihi, Kamati Kuu ya CHADEMA iliyoketi siyo Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Hii ina maana kwamba maazimio ya kuundwa kwa UKUTA ni matakwa ya Chama kimoja yaani CHADEMA. Ikumbukwe kuwa UKAWA uliundwa kwa makubaliano ya vyama vinne vya CHADEMA, CUF, NCCR-MAGEUZI na NLD. Hakuna namna yoyote ya kuwashawishi Watanzania kuwa hiki wanachokiita UKUTA ni Umoja, Umoja lazima ushirikishe pande watu zaidi ya mmoja au zaidi ya vikundi viwili au zaidi ya vyama viwili.

Mtazamo: Kabla ya UKAWA, Kambi rasmi ya Upinzani iliundwa na chama kimoja cha CHADEMA. Ni katika kipindi hicho ambapo Chadema na CUF walikuwa na msuguano mkubwa hadi kupelekea CHADEMA kuwaita CUF , CCM B huku CUF wakiwaita CHADEMA chama cha MASHOGA.

Baada ya Chadema kuondokewa na Makada wake maarufu walioshiriki kikamikifu kukijenga chama wakiongozwa na Zitto Kabwe, Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba, CHADEMA kiliyumba sana na kutafuta kila namna ya kukinusuru na anguko kuu. Ndipo Mungu aliposikiliza maombi yao na bila kutarajia, Ibrahim Harouna Lipumba akaibuka na wazo la kuundwa kwa UKAWA wakati wa Bunge Maalum la Katiba.

CHADEMA wakaingia kwenye umoja huu kwa malengo makubwa ya kufufuka jambo ambalo CUF, NCCR-MAGEUZI na NLD hawakujua. Haraka sana, Mbowe akaenda kutangaza kulivunja baraza kivuli lililokuwa na Wabunge wa Chadema pekee na kuunda jipya lenye kujumuisha Wabunge wa UKAWA. Ni katika umoja huo wa wajanja CHADEMA na mambumbumbu wa CUF, NCCR na NLD uliokipaisha chadema na kwa ujanjajanja hio CUF, NCCR na NLD wakajikuta wanamuunga mkono mgombea urais wa CHADEMA huku viongozi wa CUF, NCCR na NLD wakitumiwa kama vibaraka na wale wa CHADEMA. NCCR, NLD na CUF vimebaki majina.

Uamuzi wa CHADEMA leo wa kuuda UKUTA si chochote wala si lolote. Hizi ni hila tu vinafanyiwa vyama vya NCCR, CUF na NLD. Chadema wameona wameshajiweza, wanaamua kujivua GAMBA kutoka katika mikono ya UKAWA ili wajitegemee
Swali ni je CUF, NCCR na NLD wanalijua hilo? Wako tayari kuitwa washirika wa UKUTA wakati UKUTA umetokana na maazimio ya KAMATI KUU YA CHADEMA? Je UKUTA hautawapoteza viongozi makini kama ambavyo UKAWA ukiwapoteza akina Dr. Slaa na Prof. Ibrahim Harouna Lipumba?

Tusubiri tuone.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mbowe Na baadhi Kama yeyekatika CDM wammepanga mikakati ya kuwatosa wasiojutambua kina mbaria Na wenzake..majibu yatadhihirika kwa wasindikizaji...sinena ndiyo inaanza stelingi bado Yuko saruni anajipanga..akiingia ataanza vitu vyake.. Na dlama ya mbatia itamshtukia katika miburuzo hakuna anataka kutoswa

    ReplyDelete
  2. Wewe Mwandishi Mbona Hueleweki ?? Umetumwa au ?? Unapoandika Habari inayohusu CHADEMA, chama cha siasa kilicholeta na kuchochea mabadiliko ya maendeleo unayoona sasa ndani ya CCM ,unatakiwa uandike habari halisi NA SIO maoni yako. ULICHOANDIKA HAPO JUU NI MAONI YAKO KAMA ULIVYO ULIVYOTUMWA NA .........!! TUMIA FIKRA HATA ZA ELIMU YA MSINGI KATIKA KUANDIKA JAMBO.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Naona unaumia kwenye ukweli,mwandishi hajakosea na ana uhuru wakuandika kama wewe ulivyoandika pumba hapa,wewe ni Chadema ndio maana uko tofauti na mwandishi,mimi ni CUF nakubaliana na mwandishi.
      MAUMIVU YAKIZIDI KAMUONE DAKTARI.

      Delete
    2. Wafuasi wa chadema wanajulikana tu kwa matusi na ushari,mmojawapo wewe.

      Delete
  3. Askari wa TZ ni wastaarabu mno lakini kuna wakati naona kama mnawachokoza.Haya ngoja tuone,ila chonde tunaomba viongozi na wake zenu mtangulie mbele.

    ReplyDelete
  4. Mwandishi tunashukuru kwa mtazamo wako. Naona dalili za kufa kwa vyama vingine na pia Naona dalili cha kile kilichosemwa na jk kuwa baada ya uchaguzi ukawa itakuwa Ukiwa. Siasa zetu bado hazieleweki. Tunasafiri ndefu ktk siasa. Naona ni vyema kupinania katiba mpya Ambayo itatoa fursa ya vyama kuungana na kutengeneza chama kimoja strong Kama kweli tunamalengo ya kuiondoa ccm. Vinginevyo tule tu ruzuku maisha yetu yaende mwana nchi wa kawaida abaki tu kuwa daraja la wanasiasa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. NENO!Umenifurahisha kuliko maelezo mdau 11.36.

      Delete
  5. HATA MFANYEJE HAMNA MVUTO KAMA ZAMANI BANDUGU MPAKA MLITOE HILO LIBABU,MMENIUTHI SANA KULIKUMBATIA FISADI.

    ReplyDelete

Top Post Ad