Mama Diamond Anywea Kwa Zari Hassan

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Zari Hassan
DAR ES SALAAM: Imevuja! Baada ya muda mrefu kusambaa kwa habari kuwa mama wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassim ‘Sandra’, ‘haivi’ na mwandani wa msanii huyo, Zarinnah Hassan ’Zari The Boss Lady’, imedaiwa kuwa kwa sasa bi mkubwa huyo amenywea kwa kumkubali Zari.



Taarifa hizo zilizopenyezwa na chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya familia ya Diamond zimeeleza kuwa, hivi karibuni mama Diamond amesalimu amri na kutamka hadharani kuwa Zari ni kiboko kuliko wanawake wote ambao mwanaye amewahi kuwa nao.

“Mama Diamond kanywea kwa Zari na wala hana lolote la kusema, unajua Zari kamtuliza sana Diamond! Si kama alivyokuwa huko nyuma. Huwezi amini juzikati mama Diamond katamka kabisa kwamba hakuna mwanamke kama Zari maana amemtuliza Diamond vilivyo,” kilichonga chanzo hicho.

Baada ya kuunyaka ubuyu huo wa motomoto, Risasi Jumamosi lilimpandia hewani mama Diamond ili kumsikia anazungumziaje ubuyu huo ambapo baada kuelezwa kila kitu bi mkubwa huyo alijibu kwa kifupi na kukata simu:

“Eeeh mwanangu…eee..”

Risasi Jumamosi liliendelea kumpigia simu mama Diamond baada ya kukata lakini hakuweza kupokea tena.

Zari na mama Diamond wamedaiwa kuwa katika msuguano wa chinichini kutokana na kutoelewana tabia na kila mmoja kutomzungumzia mwenzake kwa mazuri hivyo kwa mama Diamond kudaiwa kusema anamkubali mkwewe huyo, ni dhahiri kwamba amekubali yaishe! Chanzo.GBP
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sasa mwandishi umeandika kitu gani mbona sikuelewi.

    ReplyDelete
  2. subutu.. mtajidan`ganya tuu. bi sandra anawapenda wakwe wengine sio huo alofanana nae miaka.

    ReplyDelete
  3. BI SANDRA HAMPENDI NA WALA HATOMPENDA BOSSLEBA HATA IWEJE, KAITAKA MADALE KASHINDWA SASA ANAWAGOMBANISHA DOMO NA FAMILY YAKE. TOENI UONGO WENU HAPA.

    ReplyDelete
  4. Hahahaaaaaaaa, nicheke niongeze cku za kuishi. alonywea nani? labda akaroge tena kijijini kwao ug. au kila mwaka aende Leba kupanua laki Almasi anatotoz dar.

    ReplyDelete
  5. Bossleba ni fake kuliko Wema. Bi sandra hana mpango nae labda nyie mnataka umbea tuu. Mama Zulekha fake mpaka umri.

    ReplyDelete
  6. Hapo wote njaa kali hamumwezi hata kuufikia unyayo wa zari wivu umewajaa mtabaki kusikia labda mkafute mavi yake jeaouls will kill u guys.

    ReplyDelete
  7. wewe usokuwa na njaa una nn? mbona unashinda barabarani kutafuta wateja wakugeuze upate japo mlo wa mchana huyo BossLeba hatumuwezi kwa umalya wa kuwa kila mtoto na baba yake. Shuwainnn

    ReplyDelete
  8. Hv mkiulizwa huo wivu mkubwaa kwa zari ni kitu gani eeh khaaa mwenzenu anapiga kazi maisha yana kwenda kuzaa ana zaa kaaeni vijuso kwa kushika matamaa mmeoza kwa umbea

    ReplyDelete
  9. Hv mkiulizwa huo wivu mkubwaa kwa zari ni kitu gani eeh khaaa mwenzenu anapiga kazi maisha yana kwenda kuzaa ana zaa kaaeni vijuso kwa kushika matamaa mmeoza kwa umbea

    ReplyDelete
  10. tutokee afrit mjaa laana kama zari.

    ReplyDelete
  11. tutokee afrit mjaa laana kama zari.

    ReplyDelete
  12. Dangote congratulation don't listen guys,people they are so jealous,they want misleading your family&destroy your relationship among your mother& zari,people to be provocative for diamond family is so bad.

    ReplyDelete

Top Post Ad