UKAWA Wakubaliana kuwanyima mafuta wakuu wa wilaya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameagiza wenyeviti wa halmashauri 18 nchini zinazoongozwa na Ukawa kuacha utaratibu wa kutoa fedha za halmashauri kuwasaidia mafuta ya magari wakuu wa wilaya au kuzitumia kwa ajili ya masuala ya kisiasa ya vyama vyao.

Akizungumza na mameya na wenyeviti wa halmashauri zinazoongozwa na Ukawa katika mkutano uliofanyika juzi mjini Arusha, Mbowe alisema viongozi hao wanapaswa kuhakikisha fedha zote zinazokusanywa na halmashauri hizo zinatumika kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Alisema katika kikao hicho cha mameya na wenyeviti wa halmashauri, wametambua kuwa kuna matumizi mabaya ndani ya Serikali, mbali na wafanyakazi hewa ambao wapinzani wamekuwa wakilalamika tangu mwaka 2005.

Mbowe alisema bado kuna halmashauri ambazo zimekuwa zikitumia fedha kufadhili ofisi za wakuu wa wilaya na chama tawala, jambo ambalo sasa kwa halmashauri za Ukawa halitakuwapo.

“Maeneo ambayo wakuu wa wilaya wamezoea kuomba fedha za mafuta na CCM wamekuwa wakiomba fedha kwa ajili ya kazi zao tunawaambia wasithubutu tena kwenda kwenye halmashauri zinazoongozwa na Ukawa, kwani hatutawapa fedha na tunawaumbua,” alisema.

Mbowe alisema katika halmashauri za Ukawa hawataki kusikia kuna fedha zimetolewa kwa wakuu wa wilaya au chama chochote cha siasa.

Alisema katika kikao hicho wamekubaliana kuanzisha mipango mikakati ambayo itawezesha kubuniwa vyanzo vipya vya mapato ambavyo ni rafiki kwa wananchi, kupatikana kwa ajira na kuboresha huduma muhimu za Watanzania.

Akizungumza baada ya maelekezo hayo, Mwenyekiti wa Madiwani Chadema nchini ambaye pia ni Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro alisema watatekeleza na hawatakubali kuingiliwa na wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa na makatibu tawala.

Calist alisema katika halmashauri za Ukawa uamuzi wa mwisho wa uendeshaji wa halmashauri utafanywa na madiwani na siyo mtu kutoka nje ya halmashauri hizo.

“Tutasimama na kutetea mamlaka ya kisheria ya Serikali za mitaa hapa nchini,” alisema.

Katibu wa Madiwani wa Ukawa nchi nzima ambaye ni Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob alisema watahakikisha wanasimamia utendaji mzuri wa halmashauri zote wanazoziongoza ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. UKAWA Serikali ndani ya serikali yeto macho!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. UKAWA Serikali ndani ya serikali yetu macho!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  3. Hahahahahaha!wacha nicheke anonymous.9.22.UKAWA serikali ndani ya serikali.Hawa jamaa wako vizuri kwenye kugusagusa maana duh,hili halijaisha wanazua jipya.Hofu yangu wakishika dola watasema asiekuwa mwanachama wa UKAWA asipate huduma.Mungu wetu na apishilie mbali.

    ReplyDelete
  4. Hii ndio demokrasi made in UKAWA sasa hizo pesa mbona zinakusanywa kutoka kwa wananchi wa vyama vyote kuleta maendeleo sasa huo ubaguzi una toka wapi na mikwara isio kuwa na tija basi na serikali ya CCM isitoe ruzuku kwenye halimashauri zilizo shikwa na UKAWA kuchangia maendeleo wajichangishe wenyewe

    ReplyDelete
  5. Patamu hapa
    Mafuta ya madc kwani hawana fungu Lao
    Hata mafuta ya mwenge futa yote kwanza hauna manufaa
    Viongozi wote wa mwenge wanatoka ccm kwanini ?

    ReplyDelete

Top Post Ad