Habib Mchange Amshukia Julius Mtatiro, Adai Amemgeuka Prof Lipumba Baada ya Kumfikisha Hapo Alipo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwanasiasa Habib Mchange Amemshukua Julius Mtatiro kama ifuatavyo:

"Siasa bwana wakati mwengine hovyo kabisa.
Eti Leo ‪#‎JULIUSMTATIRO‬ aliyechukuliwa na ‪#‎Lipumba‬ baada ya kuhitimu UDSM na Hekaheka za serikali ya wanafunzi DARUSO na kutelekezwa na Mnyika na Chadema anamwita #LIPUMBA msaliti!

..Duh kweli shikamoo Siasa,
Lipumba huyu huyu aliyempa Ukurugenzi wa sheria na haki za Binaadamu cheo kilichokuwa kikishikiliwa na Mbarala Maharagande Leo amemsaliti aliyemteua na kumpa mshahara kama njia ya kuwatia moyo vijana waliokuwa vyuoni wakifanya harakati.

Yaani #LIPUMBA aliyempa ‪#‎MTATIRO‬ unaibu Katibu Mkuu wa CUF from nowhere akimtosa ‪#‎WILFREDLWAKATARE‬ na kumpa muhitimu wa chuo kama chachu ya kuwatia vijana wengine Siasa bila kuwa na uzoefu wowote katika Siasa Leo amegeuka MSALITI mbele yake? ...
Kweli ukiwa unafanya Siasa uwe na ngozi ngumu aisee.

Ndio mana siasa inahusianishwa na uongo uongo na maneno mengi
Ukianza kuongea saaana unasmbiwa usilete siasa hapa. Ukiwa kigeugeu unaambiwa usilete siasa hapa.

Na Ndio mana naelewa Sasa kwanini #Mtatiro aliweza kuandika makala tuliyoipenda Sana ya ‪#‎NJAAMPAKAmakanisani‬ akiwalaumu viongozi wa Dini wanaopokea pesa za Lowassa lakini baadae akasimama kidete kumnadi huyo huyo Lowassa.
Nazidi kuelewa aisee. Siasa haihitaji uwe mkweli, ni kuongopa tu mwanzo mwisho ukisema ukweli inakula kwako.

Ni kama yule aliyewashauri watu wa Arusha wamzomee Lowassa kwa sababu ni Fisadi lakini alipohamia Chama chake akasimama kumnadi.

Ama yule mchungaji aliyesema "atakayemuunga mkono Lowassa akapimwe akili "...miezi michache baadae akawa mpiga debe wake Mkuu na fulana zenye picha yake akavaa.

Mwishowe watu wenye akili timamu watawadhalau wanasiasa kwa Unafiki wa namna hii.
Ndimi"

Habib Mchange
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad