HATIMAYE Mbunge Godbless Lema Aachiwa Kwa Dhamana

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema amepandishwa mahakamani katika kesi mbili tofauti.

Kesi ya kwanza namba 351/2016 anatuhumiwa kumtumia ujumbe wa simu wa uchochezi Mkuu wa mkoa Arusha, Mrisho Gambo wenye maneno kuwa “Karibu tutakudhibiti kama mashoga walivyodhibitiwa Uarabuni”

Kesi ya pili namba 352/16 Lema anatuhumiwa kuhamasisha maandamano Septemba Mosi kinyume cha sheria.

Hakimu amepinga hoja za wakili wa Serikali,  Vincent Njau kuzuia dhamana kwa sababu za kiinterejensia kwa usalama wake.

Lema amekana mashitaka yote, na ameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ambapo kwa shitaka la kwanza alitakiwa kupata mdhamini na shilingi 10, na shitaka la pili dhama ni shilingi milioni 15.Kesi hiyo itatajwa tena Septemba

Hakimu anayesikiliza kesi ni Desderi Kamugisha wakati wakili wa serikali akiwa ni Innocent Njau.

Baadaye vurugu ziliibuka mahakamani wakati polisi wanataka kumpeleka Lema magereza kwa madai kuwa wadhamini wamechelewa, lakini mbunge huyo alipinga hatua hiyo kwa maelezo muda wa mahakama saa 9.30 ulikuwa bado.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Yale makelele niliyoyasikia kwenye redio anapiga kelele acheni waniue nikazikwe kwetu machame ilikuaje kwani!!? yuko mzima kabisa kweli au ameumia!?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unalana wewe na mama yako
      Na wote walio furahia mbunge wetu kuonewa

      Delete
  2. Kwani wewe hujui kuwa huyu ana ule ugonjwa!! Mtu siku zote huombea kufa kwao. Na yeye pia anaonelea hivyo! Ni bora, ama sivyo?

    ReplyDelete

Top Post Ad