Lema Aendelea Kugoma kula akiwa mahabusu, Mwanasheria Wake Kufungua Kesi Mahakama Kuu Leo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), ameendelea kugoma kula kwa siku ya tatu mfululizo tangu alipokamatwa Oktoba 26 mwaka huu, nyumbani kwake mjini hapa, akidaiwa kutoa maneno ya uchochezi.

Lema alikamatwa siku hiyo saa 12 alfajiri akiwa nyumbani kwake, Njiro,  na hadi sasa anashikiliwa katika mahabusu ya kituo kikuu cha polisi mjini Arusha.

Kutokana na kuendelea kugoma kula, Wakili wake, John Mallya amesema leo saa sita mchana atakwenda Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha kufungua kesi ya kutaka mteja wake afikishwe mahakamani.

Malya jana alisema katika kesi hiyo atashirikiana na Chadema kuwashtaki mwendesha mashitaka mkuu wa Serikali na mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai, Mkoa wa Arusha.

Tangu mbunge huyo akamatwe amegoma kula kwa  kile anachodai kupinga udhalilishwaji aliofanyiwa na polisi wakati wa kukamatwa.

Pia, Lema anasema alinyanyaswa mbele ya watoto wake nyumbani kwake huku wakijua yeye ni kiongozi na amechaguliwa na wananchi.

Neema, mkewe Lema,jana alithibitisha kwamba  mumewe amegoma kula.

“Anaendelea kugoma kula mpaka sasa kwa sababu  hata sasa nimetoka polisi asubuhi kumpelekea chakula, lakini amekataa kula.

“Lakini nilipouliza pale polisi kuwa wanampeleka lini mahakamani, nilijibiwa wanaendelea kumhoji,”alisema Neema.

Juzi, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, alithibitisha kukamatwa kwa Lema na kueleza kuwa alihojiwa dhidi ya matamshi ya uchochezi na kuwa atafikishwa mahakamani baada ya kukamilika   uchunguzi.

Kwa mujibu wa Kamanda Mkumbo, Lema anatuhumiwa kuwachochea wakazi wa Arusha kuandamana Septemba mosi, mwaka huu kuhamasisha kile kinachoitwa Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta).
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jamani kama mtu unajijua una familiar. .yanini wewe kuanzisha fujo?hujui hizo fujo zitaweza kuangukia ktk familia yako? Sasa ona unavyowapa familia yako tabu mke na watoto wako. ..Mwenyezi Mungu Habariki mwenye kuvuruga amani. .huwo udicteta mnaosema kafanyiwa nani?..Mh Magufuri kwa kutaka masikini nae spate milo 3 eti dicteta .Hamna haya na mmeiweka Dunia mbele na utu wa mwanadamu nyuma

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nani amekuambia ameanzisha fujo? Alikamatwa nyumbani kwake saa 12 alfajiri sasa fujo alianzisha wapi? Tafuta katiba ya tanzania ujue sheria na muongozo wa nchi.. ijue haki yako usiichi kama bendera kufuata upepo.
      Sijui mijitu mingine mkojee?

      Delete
    2. Mnatumia mapungufu ya sheria na katiba kufanya vurugu na uchochezi. Sasa kinachomfanya agome kula ni nini. Si katiba na sheria zilizopo zinamruhusu kula, basi na ale. Kumbe kitanda cha hospitali huwa kina nafuu kuliko mahabusu. Na atagoma sana kula na maisha yanaendelea vilevile.

      Delete
  2. agome na kutundikiwa dripu pia na kukojoa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hahahahah,Yuko tayari kwa lolote?????????Anatingisha kibiriti tu kufa anaogopa sana.

      Delete
  3. Hana njaa huyo akaulize somalia ,anatafuta kiki magufuli wanyooshe hao wameshaishiwa Sera sasa wanahaha !!!! Nabado watanyooka tuuu

    ReplyDelete
  4. Hana njaa huyo akaulize somalia ,anatafuta kiki magufuli wanyooshe hao wameshaishiwa Sera sasa wanahaha !!!! Nabado watanyooka tuuu

    ReplyDelete
  5. Hana njaa. Ikimshika atakula

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kunya mnye nyie wenye kuongea sana kama mmemeza cd, akinya bata kaarisha!!! ongeeni sana ila tendeni haki hata kidogo basi da!!!

      Delete

Top Post Ad