Nuh Mziwanda asema jina la wimbo ‘Jike Shupa’ ni wazo la AliKiba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mkali wa wimbo ‘Jike Shupa’ Nuh Mziwanda amefunguka kwa kusema kuwa wazo la jina la wimbo huo alikuja nalo AliKiba.

Muimbaji huyo ambaye alikiri wimbo huo kumwimbia aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Shilole, amekiambia kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz cha EATV kuwa hakuwa na wazo la jina la wimbo huo mpaka AliKiba alivyozungumzia ‘Jike Shupa’ kwenye chorus na wimbo huo.

“AliKiba ndiyo kila kitu, yeye ndiye aliyetoa neno la ‘Jike Shupa’,” alisema Nuh. “Wimbo kanikuta nimeshaurekodi na nimeshafanya chorus yangu, na sikutaka kuiachia nikaenda kumshirikisha AliKiba akaniambia nyimbo imekamilika nitaingiza nini humu, na nyimbo nzuri nikamwambia no, kwa sababu nimekaa kimya muda mrefu nahitaji utofauti kwa sababu sijawai kufanya kolabo, basi akasema okey, tukaenda studio tukamute chorus yangu AliKiba akaingiza yake, ambapo katika kuandika kwake akaimba neno ‘Jike Shupa’, kwa hiyo tilte ya nyimbo Ali anahusika,”

Wimbo huo umefanya vizuri katika vituo mbalimbali vya radio na kumtambulisha rasmi Nuh Mziwanda katika muziki wa bongofleva.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad