Salamu ya Maalim Seif yabamba Mitandaoni Nchini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 Picha inayomuonyesha Maalim Seif Sharrif Hamad akiwa ameinama mikono ikiwa tumboni, huku Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein akiwa amenyoosha mkono kuashiria kutaka kusalimiana na katibu huyo mkuu wa CUF, sasa imekuwa moto mtandaoni.

Picha hiyo ilichukuliwa wakati wa shughuli za mazishi ya Rais wa Pili wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi kisiwani humo mapema wiki hii, na sasa inaigizwa na watu wa kariba tofauti wanaotuma mitandaoni picha inayofanana na tukio hilo.

Picha hizo zinaonyesha watoto, vijana na hata watu wa makamo wakiigiza tukio hilo.

Wawili hao walipambana kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais wa Zanzibar uliofutwa na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salim Jecha Oktoba 28, siku ambayo alitakiwa atangaze mshindi wa mbio za urais. CUF ilisusia uchaguzi mpya uliotangazwa na Jecha.

Vitendo hivyo vya kuigiza matukio ya watu muhimu sasa vimepamba moto mitandaoni. Miongoni mwa matukio yaliyoigwa sana mitandaoni ni la waziri wa zamani wa kilimo, Steven Wasira kupiga picha akiwa hajafunga vizuri vifungo vya koti na Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe kudondoka.

Pia tukio jingine lililoigwa sana ni la Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kuonekana amekaa kwenye kiti pembeni ya barabara akiongea na simu huku msafara wake ukiwa unamsubiri.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hii kali yote ni sababu ya kuukosa uraisi kama kweli maalim ni mpenda haki na mwisilamu usiye mnafiki kumbuka maalim uongozi ni majaaliwa aliye mpa yeye Shein ndo aliyekunyima wewe kama angependa kukupa wewe hakuna wakumzuia alitakalo Mwenyezi Mungu apende asipende Shein wewe maalim ungekuwa raisi lakini mola sio chaguo lake wewe kwa hiyo salamu haigombi

    ReplyDelete

Top Post Ad