Wenye Akaunti ‘Feki’ Mitandaoni kukiona - TCRA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MAMLAKA ya Udhibiti wa Mawasiliano hapa Nchini (TCRA) imewaonya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaojisajili katika mitandao hiyo kwa kutumia majina na taarifa za uongo, anaandika Charles William.

James Kilaba Kaimu Mkurugenzi wa TCRA amesema, vitendo vya watu kujisajili katika mitandao ya kijamii kwa kutumia majina na taarifa zisizo sahihi, ni kosa kisheria na kwamba wanaofanya hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Kilaba ameyasema hayo leo, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuongeza ufahamu kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao ambayo inasimamiwa na Kitengo cha dharura cha kuitikia matukio ya usalama kwenye mitandao hapa nchini (TZ-CERT).

“Tumeamua kuzindua kampeni hii ili kuwasaidia wananchi kuepuka makosa ya kimtandao na kuepuka kufanyiwa utapeli au wizi mitandaoni kwa sababu matukio mengi ambayo yamekuwa yakiripotiwa au kulalamikiwa yanazuilika kwa watu kupewa elimu ya matumizi sahihi ya mitandao,” amesema Kilaba.

Kampeni hiyo ya kuongeza ufahamu kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao, itafanyika kupitia matangazo ya redio, televisheni, magazeti pamoja na mitandao ya kijamii ambapo katika mitandao ya kijamii itajulikana kama, “Darasa mtandao”.

“Miongoni mwa mambo ambayo tutawafundisha wananchi ni kutoweka wazi taarifa zao binafsi zote katika mitandao, kubadili na kutunza neon la siri (password), kutojibu ujumbe unaosema umeshinda bahati nasibu na mengineyo mengi,” amesisitiza Kilaba.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sawa Sawa Kilaba, TCRA ni Mamlaka kamili.. Uwezo wa Kujiendesha na Kanini mnazo.. Na mnaweza Kuziboresha kila Changamoto na michakato na ubunifu mpya zina dhihiri,, Na jukumu la kuilinda na ku ielimisha Jamii Mnalo.. Kazi yenu ni nzuri na ulinzi wenu kwa Jamii ni wa kustahili pongezi.. Asante Sana

    ReplyDelete

Top Post Ad