Chadema kutoa msimamo wa Oparesheni UKUTA Leo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwezi mmoja baada ya Chadema kusitisha Operesheni Ukuta kupinga inachokiita ukiukwaji wa haki za binadamu na ukandamizaji wa demokrasia, leo inatarajia kutoa mwelekeo wa mkakati huo.

Operesheni hiyo ilipangwa kuzinduliwa Septemba mosi nchini kwa maandamano na mikutano ya hadhara kama maazimio ya Kamati Kuu ya Chadema, baada ya chama hicho kukumbwa na vikwazo kadhaa kuendesha shughuli zake, ikiwa ni pamoja na kuzuiwa kufanya mikutano ya hadhara.

Siku moja kabla ya kufanyika kwa operesheni hiyo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alitangaza kuisitisha kwa mwezi hadi kesho, ili kutoa fursa kwa viongozi wa dini kusemezana na Rais John Magufuli na Serikali yake.

Jana, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema: “Kuhusu Ukuta, kesho (leo) tutatoa msimamo wetu juu ya kitu tutakachofanya.”

Alisema operesheni hiyo ilisitishwa kutokana na sababu za msingi zilizoelezwa, hivyo kauli ya chama hicho leo itafafanua kwa kina kuhusu mambo yote yaliyojitokeza katika kipindi hicho cha mwezi.

Wakati viongozi hao wakieleza hayo, hadi jana hakukuwa na taarifa zozote za kufanyika kwa kikao kati ya viongozi wa dini na Serikali.

Viongozi hao waliitaka Serikali na Chadema kufikiria amani ya nchi na kutafuta njia mwafaka za kumaliza msuguano wa kisiasa hasa baada ya chama hicho kushikilia msimamo wake wa kufanya mikutano na maandamano.

Wakati Chadema wakijipanga kutoa tamko lao, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda jana alisisitiza kuwa Oktoba mosi ni Siku ya Kupanda Miti jijini humo ambapo viongozi mbalimbali watahudhuria.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. BOMOENI TU HUO UKUTA BHANA!
    TUJIULIZE BAADA YA UKUTA NINI KITAFUATA?

    ReplyDelete
  2. Mshindwee na mlegee,ukuta jengeni majumbani kwenu huko.

    ReplyDelete
  3. Ahaaaa! mfereji is next Drama. sema stelingi atakuwa mwingine

    ReplyDelete
  4. Si mnyamaze tu hata mkiulizwa,kwani kila kitu mpaka muongelee.

    ReplyDelete
  5. Kwa kuwa hawana kazi ya kufanya, wakaandamane na wake na mahawara zao.........mfyuuuuuuuu

    ReplyDelete

Top Post Ad