HALI ya afya ya Spika mstaafu, Samuel Sitta si nzuri..Apelekwa Nchini Ujerumani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

HALI ya afya ya Spika mstaafu, Samuel Sitta si nzuri,baada ya Serikali kumpeleka nchini Ujerumani kwa matibabu zaidi.

Habari za uhakika  zinasema Sitta alipelekwa Ujerumani juzi kwa matibabu baada ya afya yake kubadilika ghafla.

“Nilimtembelea siku moja kabla ya kupelekwa nje ya nchi, kwa kweli hali ya afya yake ilikuwa imedhoofu, namwombea Mungu amsaidia apone haraka ili arudi kuendelea na majukumu yake.

“Nimesikitishwa mno na taarifa za kuzushiwa kifo mzee wangu huyu, Mungu ni mwema najua bado anampigania uhai wake…hii tabia ya mitandao ya kijamii kumzushia mtu kifo sijui inafaidika nini.

“Mpaka anaondoka nchini kwenda matibabu natambua amekuwa asikumbuliwa mno na tatizo la miguu, sasa mimi si daktari wake siwezi kuongeza zaidi,”kilisema chanzo chetu.

Septemba 19, mwaka huu, Rais Dk. John Magufuli alimtembelea Sitta hospitalini alikolazwa kwa muda sasa kumjulia hali, kisha kumwombea dua Mungu amsaidie.

Siku iliyofuata Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa naye alimtembelea hospitalini kumjulia hali.

Sitta ameshika  nyadhifa mbalimbali, zikiwamo za Spika wa Bunge kuanzia mwaka 2005 hadi 2010, uwaziri na ubunge kwa kipindi kirefu.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Miguu mbona ugonjwa wa kawaida ulaya
    Ugonjwa huwapata watu wengi wafikiapo miaka 50 na kuendelea
    Ulaya watu wenye matatizo haya guava viatu maalumu au viatu vyenye soli maalum au silicon
    Mzee si mtoto mdogo
    Ujerumani ndo maaarufu duniani hakuna
    Upo wapi mzee
    Munich,Berlin au Hamburg
    Watu tuje tukuone

    ReplyDelete
  2. Miguu mbona ugonjwa wa kawaida ulaya
    Ugonjwa huwapata watu wengi wafikiapo miaka 50 na kuendelea
    Ulaya watu wenye matatizo haya guava viatu maalumu au viatu vyenye soli maalum au silicon
    Mzee si mtoto mdogo
    Ujerumani ndo maaarufu duniani hakuna
    Upo wapi mzee
    Munich,Berlin au Hamburg
    Watu tuje tukuone

    ReplyDelete

Top Post Ad