Hivi Ndivyo Nilivyofanikiwa Kujiajiri Baada ya Kumaliza Chuo Kikuu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kwenye kitabu kimoja nilichowahi kusoma, kuna habari ya jeshi lilokwenda vitani. Baada ya wanajeshi wote kuvuka daraja kuwaelekea maadui jemedari mkuu akaamua kuchoma moto lile daraja, magari na kila kitu ambacho kingewawezesha kukimbia ikiwa vita ingewaelemea.

 Kisha akawageukia wanajeshi wake akawaambia, "Chagueni kushinda vita ama kufa kwa sababu kukimbia ama kurudi nyuma haiwezekani tena". Jeshi lile lilishinda vita! Mbinu hii nimepata kuitumia nilipofanya rasmi maamuzi ya kujiajiri pindi nilipomaliza chuo kikuu.

 Nilijua kwenye kujiajiri kuna changamoto nyingi na kuna hatari nikakata tamaa na kutafuta ajira. Nikaamua kuchoma madaraja yote yanayoweza kunifanya nikimbie kujiajiri kwenda kuajiriwa! Kwanza kwa makusudi sikuchukua cheti cha matokeo wala cheti chochote wala barua inayothibitisha nimemaliza chuo kikuu; pili nilijiapiza kutoshughulika na matangazo, habari ama taarifa zozote kuhusu ajira. Nikabaki na option moja tu ya kuhakikisha napambana kufa na kupona kwenye kujiajiri mpaka kieleweke.

 Haikuwa kazi rahisi, lakini sikuwa na namna zaidi ya kutoka ama kufa. Nilikataa kufa na leo ninasonga mbele kwa mafanikio. Ninachokuhakikishia ni kuwa ukiamua kwa moyo mmoja kufanikiwa katika jambo lolote; ni lazima utafanikiwa, no matter what!! Kama stori nzima haijakuvutia, chukua sentensi moja ya mwisho!

 By SmartMind
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Enter your comment...sasa alijiajir kwenye biashara gani ili jamii ijifunze kutoka kwake. hajasema alianzaje na sasa yuko wapi. habar haina mashiko mwandish uwe unaweka habar za maana kuliko hii ambayo haijakamilika

    ReplyDelete
  2. Kwa upande wangu naona kama vile siyo true stori, kikubwa mwandishi alikuwa anataka kufikisha ujumbe kwa msomaji suala zima la kujituma katika maisha ili ufanikiwe na hususani kwenye kujiajiri, kwani watz wengi tu waoga kujiajiri kila siku tunawaza kuajiriwa.

    ReplyDelete
  3. Ni kweli kabisa naungana na wewe

    ReplyDelete

Top Post Ad