Makonda Awaponda Wanaobeza Jitihada za Rais Magufuli, ‘Hawajui Wanalolitaka’

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemmwagia sifa Rais John Magufuli kwa utendaji wake na kusema yeye ni mtu wa kutenda na sio maneno huku akiwapa vidonge vya wale wanaobeza jitihada zake.

Makonda ametoa kauli hiyo Jumatano hii kwenye uzinduzi wa ndege mpya za ATCL kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Mheshimiwa Rais naomba uendelee kutenda, sisi tumegawanyika kwenye upande wa fikra,kuna watu ambao hawajui wanachokitaka na hata ukiwafanyie yale ambayo ulifikiriA wao wanayataka kumbe sio,” alisema Makonda.

“Ikumbukwe wakati wa bunge tulikuwa tunafuatilia kusikiliza, Tanzania haina ndege tumezidiwa katika nchi za Rwanda tumezidiwa na wapi, umenunua ndege wanaanza kusema ndege zenyewe hazijang’aa, wamekuja kuzioshea airport, hawajui nini wanachokitaka. Hao hao walipiga kelele tunataka elimu bure,angalau na wananchi wa hali ya chini wapate elimu bure, wameanza kusema elimu yenyewe bure wakati majengo yanadondoka! Kwahiyo hawajui wanalolitaka. Hawa hawa wana lalamika foleni Dar es Salaam, umeamua kutujengea barabara hizo hela za barabara ingeenda kwenye chakula tunakufa na njaa, mheshimiwa rais hawajui wanalolitaka,” alieleza.

“Sisi tunaojua tunalolitaka tupo pamoja na wewe, tunakuunga mkono usiku na mchana na tutaendelea kukuunga mkono usiku na mchana na ninaamini kwamba wanasiasa wengi wanasubiri kutimiza ahadi zao katikati au mwishoni mwa kuelekea kampeni wewe hujasubiri, uliahidi ndege mwaka jana leo hata mwaka hujamaliza ndege zimeingia, wewe ni mtendaji ambaye tutaendelea kukuombea,” alisisitiza.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Natapika na kuharisha
    Watu waliotoa huruma jana wanazungumza kitu kimoja wengine kujisifia
    Fyuu
    Wazungu wametucheka kweli
    Pale ilikuwa ni rais na balozi wa Canada tuu
    Wazungu wana sema ndo maana Africa haiendelei muda ni kitu muhimu
    Upigaji picha fyuu
    Jana rais ndiye angekuwa msemaji tens kwa risala fupi yenye maana na si vijembe na mafumbo bila kutaja ilani za CCM zile ni pesa zetu watanzania wote
    Naelewa kwanini tv ya taifa haioneshi bunge live
    CCM acheni ujinga

    ReplyDelete
    Replies
    1. HATA HUYU PIA HAJUI ANACHOKITAKA...........

      Delete
    2. mjinga ndo wewe ukawa maana unaonekana huna muda mrefu utavua nguo hadharani kwa uchizi wako na si ajabu hata kodi hulipi jizi wewe peleka ujinga na ufinyu wako wa akili kuleeeeeeeemfyuuuuuuuuuuuuuuuuuu

      Delete
    3. Hahahahahahah,mweh!Hivi nani mjinga kati yako na ccm?Leo unamkubali JPM kuwa rais?si mlisema/ulisema hamumtambui?

      Delete
    4. KUMBE WAPUUZI BADO MKO WENGI?

      Delete
    5. Kwa Wizi wa kura
      Sasa mmehamia CUF fyuu

      Delete
  2. Sherehe haikuwa na itifaki
    Tulizundua ndege zetu mpya
    Mbili toka Canada
    Wageni wakuu Canada na Tanzania
    Rais wetu na balozi wa Canada
    Watu wengine walipachikwa kisiasa pamoja na hotuba za ambazo haziandaliwa badala yake walisema wote kitu kimoja
    Wengine kutoa vijembe na mafumbo
    Angalia balozi wa Canada Tanzania
    Aliandaa speech yake
    Kwetu kila anaropoka kivyake
    Usafiri wa anga dunia nzima unautizama
    Bora hata mapilot wa ndege hizo wangepewa nafasi kuelezea jinsi gani watakavyo huduma kwa abiria
    Ingekuwa bora kuliko ya RC no one know him duniani zaid ya bongo
    Sekta ya usafiri hasa Anga ni ya kimataifa kwa sisi tuanzao
    🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿😄😄😄😄😄😄😄😄😄

    ReplyDelete
  3. KAKA HIVI HUO MUDA WA KUBISHANA NA WASIOMKUBALI MAGUFULI MNAO?HAYA,ILA USISAHAU "HAPA KAZI TU"

    ReplyDelete
  4. KULA MAJIVU KWA WINGI,UTAACHA KUTAPIKA NA KUHARISHA.

    ReplyDelete
  5. aKILI MALI. nGEGE YA MALI YA wAWATANZANIA SI CHAMA. HII NI SASA MBOVU KWA VIONGOZI WA CCM KUTOTOFAUTISHA CHAMA NA TAIFA WAPI CCM WAPI TAIFA. UFUKARA WA KUFIKIRI NDIO HUU. JAJI WARIOBA KAZUNGUMZA JANA NCHI INAENDESHWA KICHAMA SABABU VIONGOZI WAMEJICHAGUA KICHAMA HAWAONI TOFAUTI. HII NI JANGA NA HATARI LIKAENDELEO KITAIFA. CCM NI CHAMA HAPA NDUGU MAGUFULI ILIBIDI ATANBUE ANAWAKILISHA TAIFA LA TANZANIA KWA TAIFA LA CANADA. HIVI MAKONDA ANAJUA TOFAUTI ZAKE? ELIMU FINYU. KWA NINI KUJITAMBA KICHAMA AMBAPO SI CCM BALI TANZANIA.

    ReplyDelete

Top Post Ad