UKUTA Ndio Basi Tena "UMEBUMA"...Chadema Watangaza Kuairisha Tena Maandamano ya Oparesheni UKUTA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe ametangaza kuwa Operesheni UKUTA iliyokuwa ifanyike Oktoba Mosi haitofanyika tena.

Mbowe amesema hayo leo baada ya kimya cha muda mrefu tangu kuahirishwa kwa maandamano Septemba Mosi. Aidha, Mbowe amesema kuwa hawatataja tarehe ya kufanya maandamano ili kutompa adui nafasi ya kujipanga. Amesisitiza kuwa maandamano yapo, ila tarehe hawataweka hadharani.

Operesheni hii ilikuwa ifanyike Septemba Mosi mwaka huu lakini iliahirishwa ili kuwapa nafasi viongozi wa dini kuweza kukutana na kujadiliana na Rais Dkt Magufuli juu ya mustakabali wa hali ya kisiasa nchini kufuatia kuzuiwa kwa shughuli mbalimbali za kisiasa.

Hadi leo viongozi wa dini bado hawajakutana na Rais Magufuli licha ya wao kueleza kuwa Rais Magufuli hajakataa kukutana nao kama inavyoelezwa na baadhi ya vyombo vya habari

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Usitegemee sana huko. Kuna makundi hata huko. Kuna wenye mwamko na wasio na mwamko.mua siasa pia. Kuna waoga pia.bado Tanzania kifikra wengi hatujaona mbali. Tatizo ni wengi kujiona wanaelewa na wasomi lakini ni taab tu.usomi wa mubabaishia na mweleo wao ni wa hapahapa ni tatizo kubwa kwa Taifa letu. Hakuna kitu kibaya kuliko ujinga. Tukijisikia tunaelimu kumbe ujinga umezidi hata kufumbuka kutakuwa shida sababu ufahamu mdogo na kuruhusu elimu mbadala hakutafanyika. Ni kama kupiga kelele kwa kiziwi asiyesikia. Ndo nvhi yetu ilipo sasa hivi

    ReplyDelete
  2. Hahahahaha!!! Amakweli JPM sio-mtu-wa-mchezo-mchezo.............HAPA KAZI TU, maandamano KWENUUUUUU

    ReplyDelete

Top Post Ad