UTAFITI Twaweza ‘Wambeba’ Tena Magufuli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

RIPOTI ya utafiti mpya wa taasisi ya Twaweza imeeleza kuwa watanzania wengi wanaunga mkono, hatua ya Rais John Magufuli kupiga marufuku mikutano na maandamano ya kisiasa hapa nchini, anaandika Aisha Amran.

Matokeo hayo yanatokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,602 kati ya tarehe 23 na 29 Agosti, mwaka huu kwa njia ya simu. Utafiti huo ulihusisha wananchi wa Tanzania Bara pekee na kwamba watu 6 kati ya 10 wamepinga kuwa nchi inaongozwa kidikteta.

Watu hao ni sawa na asilimia 58, walipinga kuwa nchi inaongozwa kidikteta huku asilimia 31 wakieleza kutokuwa na uhakika juu ya suala hilo.

Katika utafiti huo unaopewa jina la, “Demokrasia, udikteta na maandamano” unaripoti kwamba  asilimia 80 ya watanzania waliohojiwa, wanasema  baada ya uchaguzi, vyama vya upinzani vikubali kushindwa na visaidiane na serikali kuijenga nchi.

Huku asilimia 20 pekee ndiyo wananchi wakisema wapinzani waifuatilie na kuiwajibisha serikali iliyopo madarakani.

Katika hatua nyingine, ripoti hiyo imedaia kuwa asilimia 71 ya wafuasi wa vyama vya upinzani wanaunga mkono kufanyika kwa mikutano huku asilimia 37 ya wafuasi wa chama tawala nao wakiunga mkono kufanyika kwa mikutano ya hadhara.

Aidha ripoti hiyo ya Twaweza inadai kuwa, asilimia 48 ya waliohojiwa juu ya kuanzishwa harakati za Umoja wa Kupinga Udikteta (UKUTA), wanapinga umoja huo huku asilimia 22 pekee wakiunga mkono umoja huo.

Pia asilimia 55 ya wafuasi wa vyama vya upinzani waliohojiwa, wanaunga mkono harakati za umoja huo huku asilimia 44 wakiwa hawaungi mkono na asilimia 6 ya wafuasi wa CCM wanaunga mkono juhudi za Ukuta.

Aidan Eyakuze, Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, amesema watanzania wengi wanaunga mkono mfumo wa demokrasia ya vyama vingi na uhuru wa kukusanyika na kutoa maoni.

“Hili ni jambo la kuzingatiwa na serikali kwa sasa, wananchi ya hawakubaliani na kauli inayosema kuwa Rais Magufuli ni dikteta, wanasema ili kulinda amani  na kuchochea kasi kubwa ya maendeleo lazima hatua thabiti zichukuliwe,” amesema Eyakuze.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. "HAPA KAZI TU"SIO DIKTETA KABISAAAAAA,ISIPOKUWA WA-TZ TULIZOEA KUFANYA VITU KIMAZOEA.TUFANYE KAZI KWANI TAYARI TUMEONA JUHUDI ZA SERIKALI YA AWAMU YA TANO,JAPO KUNA WALAKINI KIDOGO HASA MASLAHI KWA WATUMISHI WA UMMA & TUKIAMINI YATAREKEBISHWA.(wanasema)HUWEZI KUWA MZURI ASILIMIA 100,LAKINI JPJM NAMPA ASILIMIA 80 MPAKA HAPO ALIPOFIKIA,NASEMA KUTOKA MOYONI,MIMI NI MPINZANI LAKINI JPJM AMEIFANYA TANZANIA IWE NA ADABU,TUNAHESHIMIANA,TUNA WOGA,TUNA NIDHAMU N.K.MUNGU AKUBARIKI RAIS WANGU.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli kabisa mdau.
      Ile ya watu kukaa baa kama seating room hakuna tena,
      Ile kupata huduma za kijamii(hospital)hakuna kama sio kupungua,
      Ile kupata kazi/shule kwa kupitia mjomba hakuna tena,
      Ile ya kwenda kutumbua Dubai kila mwisho wa wiki hakuna tena,
      N.K.
      Kama mnabisha fanyeni muone.

      Delete
  2. Habari ndio hiyo,japo wako wanaolazimisha Magufuli achukiwe na wananchi.Kaza buti baba,wanyonge tuko nyuma yako.Tunakuombea kwa Mola wetu.

    ReplyDelete
  3. Tanzania itapiga hatua kubwa kama watu wanakuwa huru, wanaruhusiwa kushindana, muwa tofauti na badala ya kutii kama kondoo.tumekuwa kama mondoo toka tupate uhuru.na wengi hawajui faida ya kuwa tofauti kimawazo inaleta changamoto kubwa kimaendeleo. Wengi viongozi wakuu wamikoa wanaiga au kutimiiza maagizo ya raisi bila hata kufikiri. Na kama nchi itaendelea namna hii mutimiza kauli za raisi bila hata kuchanganua taifa limepotea, litazorota au tutaona marudio na makosa ya mara kwa mara. Sikatai wako mikoani kuhakikisha mambo yanakwenda sawa lakini inawabidi pia watumie akili zao wenyewe kusaidia mikoa na si kupokea amri.

    ReplyDelete

Top Post Ad