Diamond Aeleza kisa cha Kukataa Kusainishwa na Label ya Jay Z, Roc Nation

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Diamond Platnumz alitosa kusainishwa na label inayomilikiwa na Jay Z, Roc Nation.

Akiongea kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM, staa huyo alisema hiyo ni moja tu ya label kubwa za Marekani alizozitolea nje. “Wakati nipo BET, Roc Nation walinifuata wakitaka wanisaini,” alisema Diamond.

“Acha Roc Nation kuna baadhi ya record label nyingi sana kubwa, nyingi sana, tena hawanifuati hivi hivi, wananifuata na ofa,” aliongeza.

“Lakini kila kitu ni target, mimi siku yoyote ukisikia nimefanya kazi na label kubwa duniani, sio kuwa under record label, ila pointi yangu itakuwa kwamba kuona namna gani wanaweza kukuza muziki wangu kidunia zaidi, nitafanya kila kitu mwenyewe. Kupata collabo na msanii yeyote mimi naweza kupata sababu Kimarekani collabo sio story, hela yako, ni biashara, mtu hawezi akakupa bure mfanye nyimbo ili upate hela, ukanye show yeye anafaidika na nini?”

Kingine Diamond alisema kama ni msanii mkubwa inakuwa rahisi kupata collabo za aina hiyo.

“Nataka mtu akinisaini, nataka muziki wangu uuzike kama wanavyouza akina Jay Z, Kanye West. Sitoingia eti Diamond kaingia na record label fulani, WCB itaingia na kampuni fulani na ikiingia ni katika makubaliano ya kuuza muziki katika digital kuona ni namna gani muziki wangu utauza sehemu fulani kwa bei nzuri.”

Source:Bongo5
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kichwa cha habari na story ni tofauti kabisa....Kuna msanii anakataa kufanya kazi na J zee for realy guys....hebu danganyeni watu wengine banaa sio wale wanao kesha na kufuatilia News za music kila siku na bandle la Internet ni free sio la kuunga unga..

    ReplyDelete
  2. du! Diamond kwa masifa ndiyo mwenyewe ameshakuwa mr misifa Dully sakes, eti Diamond akatae kusainishwa na Jay-z??? Diamond muongo mkubwa tangu lini mswahili akatae kusainishwa na J-Z???. Sema Diamond bado hujaulizwa na J-Z siku akikuuliza utasaini hata bila kufikiria cha meneja wako au bila kufikiria WCB tena utasahau WCB tena utawashangaa hao kabisa na kujiuliza hao ndio kina nani

    ReplyDelete
  3. HONGERA SANA DIA!! ILA KAMA UNAVYOJUA BINADAMU HATUACHI KUSEMA. INSHALA NDOTO ZAKO ZITATIMIA WAKATI WAKE UKIFIKA

    ReplyDelete
  4. Nilivyoelewe mimi ni kuwa katoa mfano na kwa malengo gani ambayo yataweza kumfanya akubali kitu hicho... lakini watu wanabadilisha kila kitu ambocho kinaongelea issue hiyo.

    ReplyDelete

Top Post Ad