Kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Baada ya Habari Kuzagaa Ametumbuliwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Saa chache baada ya kusambaa taarifa zilizokanushwa na Ikulu zilizodai kuwa uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo umetenguliwa, Mkuu huyo wa Mkoa ameandika ujumbe mzito unaoonekana kuwalenga mahasimu wake.

Taarifa hizo zilizothibitishwa kuwa za uongo ziliibuka siku moja baada ya tukio la kusikitisha la kuzuka ugomvi wa maneno kati ya Mkuu huyo wa Mkoa na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kwenye hospitali ya mama na mtoto inayojengwa eneo ya Burka nje kidogo ya jiji la Arusha, mbele ya wafadhali wa mradi huo.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Gambo ameandika, “Mara nyingi ukisikia huyu ana kufa leo au kesho, huwa anaishi miaka mingi zaidi! Nazungumzia utamaduni wetu sisi Watanzania!”

Mvutano kati ya Gambo na Lema ulianza tangu Gambo alipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha huku kila mmoja akimtupia lawama mwenzake kwa kutofuata taratibu na protokali.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ila jamani pamoja na kwamba mimi ni mpinzani,lakini ukweli kufanya kazi na lema inataka moyo.

    ReplyDelete
  2. Gambo umetia aibu ...inaboa du

    ReplyDelete

Top Post Ad