Wanafunzi UDSM Waitupia Lawama Bodi ya Mikopo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwisho mwa wiki iliyopita wizara ya elimu ilitangaza majina ya wanafunzi watakaopata mikopo na vigezo vilivyotumika ikiwemo wanafunzi waliosoma masomo ya sayansi, walemavu, yatima, pamoja na ufaulu wa waombaji huku vigezo hivyo vikiwaacha nje wanafunzi wanaochukua masomo ya sanaa.

Wakizungumzia mabadiliko hayo, wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, UDSM, wamesema hakuna aliyetarajia kutokea kwa hali hiyo kwani hawakutangaziwa mapema kwamba utaratibu wa utoaji mikopo umebadilika. Wengine wamedai kuwa wazazi walikuwa wamekwisha wasafirisha watoto kutoka mikoani wakitegemea udhamini kutoka bodi hiyo.

Naibu waziri wa mikopo UDSM, Abdul Nondo amesema, “Ukiangalia taarifa ambayo imetoka bodi ya mikopo kwamba itatoa fedha kwa wanafunzi ambao watasoma Sayansi,itatoa fedha kwa yatima,itatoa fedha kwa walemavu wale ambao ni maskini. Wamesema shule za kata kwa kulipa ada shilingi elfu 20/70 mpaka kufika chuo sasa hivi na kufanya vizuri. Wanapewa vigezo vya kutopewa mikopo na kubaguliwa kwamba as if they are not students.”

Kwa upande wake waziri wa mikopo wa UDSM, Kasunzi Eliud alisema, “Unaweza ukafika kuna mwanafunzi wa sayansi ni daktari lakini ametokea katika familia tajiri, tunasema familia inayojiweza. Lakini mimi mtoto wa mkulima ambaye nimeweza kusoma kwa shida kwa kuungaunga pesa mpaka nikafika chuo kikuu, leo hii vigezo vinakuja kutoka kwamba mwanafunzi anayesomea masomo ya arts hawezi kupata mkopo.”
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Si mliipenda wenyewe.....vumilieni mpaka akili itakapowakaa ndo mtajua umuhimu wa box

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tulipenda kwa vipi?usichangie usichokijua au kuelewa,Ms

      Delete
  2. Rais wetu tafadhali anangalia hili,wanafunzi wote wapate mikopo kwa nini wabaguliwe?Bora muache kujenga madaraja,hela ziende kwenye hospitali na mikopo kwa wanafunzi."HAPA KAZI TU"

    ReplyDelete
  3. Kwanza hii tabia ya ubaguzi sijui imetoka wapi tabia mbaya sana mkopo kila mwanafunzi aliyefauli kwa haki apewe siyo kutuletea sijui mtoto wa familia bora au wa mkulima mpuuzi mtupu. hivi unawezaje kumuacha mtoto aliyefaulu kwa kiwango cha juu eti kisi amefaulu ARTS acheni siasa kwenye elimu mkopo si bure atakuja ulipa mpeni kama kweli anastahili

    ReplyDelete

Top Post Ad