Bashe Adai Lowassa Alionewa CCM, Aeleza Uhusiano wao Kwa Sasa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mbunge wa Nzega, Hussein Bashe (CCM) amesema kuwa anaamini waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa aliondolewa kwa kuonewa katika mchakato wa kugombea urais ndani ya CCM.

Bashe amesema kuwa kitendo hicho alichokiita cha kiuonevu ni changamoto kubwa ndani ya CCM na kwamba wengi wameonewa katika michakato ya kuwania nafasi mbalimbali.

“Yaliyomkuta Lowassa yamewakuta wengi ndani ya CCM, hivyo jambo hilo sio geni,” Bashe anakaririwa na Mwananchi. “Wapo waliobaki na wapo walioamua kuhama chama kwa sababu ni binadamu. CCM ina historia hiyo, hii ndiyo changamoto yake kubwa,” aliongeza.

Mbunge huyo alifafanua kuwa kwakuwa Lowassa alituhumiwa kwa mengi ndani ya chama hicho, alipaswa kuitwa na kuelezwa tuhuma zake na sababu za kuondolewa jina lake ili umma ufahamu.

Alisema kuwa katika chama hicho, kashfa nyingi hufanywa kwa sababu maalum na hubuniwa kwa ajili ya kufikia lengo fulani dhidi ya mtu au kikundi cha watu.

Alisema kuwa mbali na sakata la Richmond lililopelekea Lowassa kujiuzulu nafasi ya uwaziri mkuu, masakata ya Lugumi na Tegeta Escrow ni sehemu yale yaliyobuniwa kwa lengo maalum.

“Tazama wanavyofunika sakata la Lugumi. Usiende mbali angalia sakata la Escrow. Tumeadhibu waliopata fedha kutoka benki ya Mkombozi, vipi wa Stanbic? Wizi mwingine uliofanywa nchi hii una uhusiano kati ya Serikali na vikundi vya watu wenye uhusiano na Serikali,” Bashe aliliambia Mwananchi.

Akizungumzia uhusiano wake na Lowassa ambaye alikuwa anamuunga mkono wakati wa mchakato wa kugombea urais kupitia CCM, Bashe alisema hivi sasa hawana uhusiano tena wa urafiki wa kisiasa.

Alisema kuwa alimshauri sana Lowassa kutohama CCM, avumilie, lakini hakufanikiwa kumshawishi, hivyo waliagana.

“Lowassa ni mzee wangu. Ni mtu ambaye namheshimu na nitaendelea kufanya hivyo, ingawa kwa sasa hatuna uhusiano wa kisiasa,” alisema.

Lowassa alihama CCM baada ya jina lake kukatwa katika mchakato wa kuwania urais, alihamia Chadema na kupewa nafasi ya kugombea urais katika uchaguzi unaotajwa kuwa na ushindani mkali zaidi tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hivi kweli huu ni wakati wa kukaaa na kumzungumzia Lowassa. Mbona hayo maneno yaliisha pitwa na wakati sana na HAPA KAZI TU inaendelea. Nilitegemea Kada Mzima kama wewe wa Chama husika ungekaaa hapo na kuyazungumzia maendeleo na changamoto mnazokutana nazo kama Chama katika kuyakamilisha hayo Maendeleo yanayotokana na ilani za Chama chako mwenyewe. Kweli akili ni nywele na kila mtu ana zake. Sasa Kada mzima badala ya kutuelezea Ilani ya Chama kwa ajili ya Maendeleo ya Wananchi na hasa wale Wananchi maskini na wenye kipato cha chini wewe unabakia kutuletea Habari za Mtu. Tena mtu aliyeshindwa siasa. Kwa kweli majipu bado ni mengi Nchi hii!!!

    ReplyDelete
  2. Hongera Mhe. Bashe kwa kuongea Ukweli. Hata sisi wananchi tuna mengi tusiyoyaelewa yanaibuliwa na kuishia hewani na kutuacha tukidhani kuna mkono wenye nguvu zaidi. Ifike wakati hata Kiongozi wa juu kabisa wa nchi akifanya madudu sheria ichukue mkondo wake tuache hiazi mambo za kubebana na kukandamiza wadogo!

    ReplyDelete
  3. Sidhani kama hayo maneno Bashe aliyasema kipindi hiki cha HAPA-KAZI-TU, nadhani mwandishi aliyaweka kama akiba kwa matumizi ya baadae, ili kuvuruga hali ya hewa - USHINDWE NA ULEGEE......

    ReplyDelete

Top Post Ad