KHADIJA Yusuph Amtaka Leila Rashid Aachane na Mambo ya Kidunia na Kumfuata Mumewe Mzee Yusuph

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msanii wa taarabu nchini Khadija Yusuph amemsihi wifi yake Leila Rashid kuachana na maswala ya muziki na kumfuata mume wake Mzee Yusuph kwa kuwa tayari mume wake kashaenda hija na ni dhambi kuacha kumsikiliza mume wake.

Akiongea ndani ya eNewz Khadija amesema ni vizuri Leila kumfuata mume wake kwa kuwa haoni sababu ya yeye kuendelea kuwa na kundi la Jahazi wakati mume wake Mzee Yusuph ameamua kumrudia Mungu na kuachana na maswala ya muziki.

Hata hivyo Khadija Yusuph amewaambia mashabiki waendelee kusubiria maamuzi ya Mzee Yusuph mwenyewe juu ya maamuzi ya mke wake kuendelea na muziki wakati yeye kaamua kumrudia Mungu na kuachana kabisa na mambo ya dunia.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. 1. Kwanza mambo ya imani sio ya kulazimishana. Wifi usimshinikize wifiyo. Kwanza muziki sio dhambi.. dhambi ni yale matendo ndani ya muziki wenu yasiyompendeza Mungu. 2. Sasa wote wa kuacha pesa it atoke ktk biashara gani?

    ReplyDelete
  2. huyo wifi ana wivu na Leila sababu Leila ana kipaji kikubwa sana kumshinda yeye na Leila anajua kuimba nazipenda sana nyimbo zake lakini huyo wifi yake ingawa na yeye ni mwimbaji lakini sijawahi kumsikia

    ReplyDelete
  3. khadijah yusuf ndio kiboko kama hujamsikia kauluze wanaomjua kila moja wao ana kipaji chake wacheni kuendeleza chuki

    ReplyDelete
  4. KWA IMANI YA DINI YA KIISLAM NI KUWA MWANAMUME ANATAKIWA KUMUARISHA MEMA MKEWE KWANZA PAMOJA NA WALIOMO NDANI, HAILETI PICHA NZURI MUMEO AMEACHA MAMBO YOTE YASIYO NA MAANA WEWE UNAENDELEZA? NA MUME AMESHINDWA KUMDHIBITI MKEWE, YEYE ANAKULA KIYAMU LAYLI MKEWE ANATOKA KWENDA KWENYE SHOO USIKU? ALLAH AWAZINDUE ZAID IN SHAA ALLAH. NA PIA KATIKA DINI YA KIISLAMU MZIKI NI HARAMU NA NI KATIKA MAMBO YA IBLIS LAANATULLAH!

    ReplyDelete
  5. Ilibidi nawe uache huo mziki kisha umshauri wifi yako hapo tungekuelewa

    ReplyDelete

Top Post Ad