ALICHOANDIKA Darassa Baada ya Dereva Kukamatwa Akicheza Wimbo Wake Huku Akiendesha Gari

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msanii wa Bongofleva Darassa ambaye kwa sasa anafanya vizuri na hit single ya wimbo wake mpya unaoitwa ‘Muziki’ ameamua kuweka wazi mtazamo wake kuhusu ile video iliyosambaa ikionesha vijana wakicheza wimbo wake  huku dereva akiacha  gari likienda.

Vijana hao wamekamatwa na polisi na Darassa ameamua kutoa mawazo yake kuhusiana na kitendo hicho ambacho kimewafanya vijana hao kukamatwa na polisi Itigi Singida, Darassa ametuamia account yake ya instagram kuandika ujumbe kuoneshwa kuguswa na

“Hawa ndugu zetu nimepata taarifa wamekamatwa kwa kosa la kutaka kusababisha ajali na unaweza kuona Kama mchezo ulielekea kubaya, ingeweza kua Tatizo kwao Au kumu sababishia mwingine, Naskia watakua mahakamani Leo I’m not so sure naendelea kufatilia”

“Nawaombea Tatizo hili Mungu awafanyie wepesi I’m sure wamejifunza Hawawezi kufanya tena mistake Kama Hii itokee, mizuka feelings mtu anaweza kufanya kitu njee ya mipango yake sometimes, Mungu awasaidie 🙏🏽 LENGO NI KUJENGA DUNIA KUA SEHEMU NZURI NA SALAMA KUISHI #Muziki“
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Unafuatilia kitu gani mjinga wewe; fanya yako. Wewe endelea kujitahidi na mziki wako usiokuwa na kichwa wala miguu. Mambo ya sheria za usalama barabarani waachie Polisi pamoja na vyombo vingine vya usalama barabarani pamoja na Mahakama. Hivyo vitu havikuhusu na elimu yako ndogo.

    ReplyDelete
  2. Wewe ndo mjinga tena wa kutupwa,Darassa fuatilia hao ni mashabiki wako na unajua mzuka ulivyo achana na watu mawivuu tuu yamewajaa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kuwafuatilia pekeee kutasaidia nn wakati mashabiki wenyewe ni wajinga kwa kukiuka sheria za usalama barabarani. Je kama wangesababisha vifo ingekuwaje?????......acha upumbavu wewe mchangia hoja. Na wewe ni yule yule.........

      Delete
  3. kwa hiyo ndugu Amani unafikiri walichokifanya vijana hao ni sahihi eti kwa sababu ni mashabiki wa Darasa? Amani naomba acha ushabiki wa kijinga ndugu yangu, hivi ikitokea ajali unadhani wa kuadhirika ni hao vijana pekee? ni wao pekee wanatumia barabara?? ni mara ngapi tunapoteza wapendwa wetu kwa ujinga kama huo na mengine? au unataka Daraasa afuatilie ili akumbane na mkono wa shria kuwa yeye ndiye aliwatuma wafanye hayo? kimsingi kama msanii anatakiwa afanye yake na ikibidi akemee mambo waliyofanya hao, sawa ndugu AmaniMtui??? tuijenge Tanzania ya Amani

    ReplyDelete
  4. Darassa huna influence hapo. Hata usipofatilia sheria itachukua mkondo wake. Kwahiyo uko Singida au ?! Hahahaha. Kama huna cha kuandika kaa kimya.

    ReplyDelete

Top Post Ad