CHID Benzi Aonekana Live Akibwia Unga..Mwenyewe Adai Uvimbe Alionao ndio Sababu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mtandao wa Global umeripoti habari waliyoifanyia uchunguzi na hadi kufanikiwa kumnasa Chid Benz Kwenye Chumba cha Hotel anayoishi...
.
Mtandao huo umeripoti hivi:

DAH, KUMBE CHID ANAUMWA HERNIA

Aliposogea, OFM lilimlaki kwa shangwe na kumchangamkia kiasi kilichomfanya atulie, akae chini na kuanza kupiga stori kwa zaidi ya saa moja, huku mara kwa mara akilalamika kuwa anaumwa sana ugonjwa wa Hernia na pia uvimbe chini ya kitovu ambao unamsababishia maumivu makali.  Chid alikuwa ameshika karatasi mkononi iliyoandikwa namba za simu za prodyuza Lamar ikadondoka chini, katika hali ya kushangaza alishindwa kuiokota maana kila alipoinama alihisi maumivu makali. OFM wakamsaidi a kuokota karatasi hiyo.
.
Chid: Washikaji msione nipo hivi lakini kiukweli ninaumwa sana, ninaweza kufa muda wowote, huu uvimbe chini ya kitovu unaniuma sana (akatoa wembe na kutaka kuuchana huo uvimbe, OFM mmoja alimdaka na kumsihi asifanye hivyo, akakubali baada ya kubembelezwa kwa muda).
.
OFM: Lakini kwa nini sasa unabwia unga na upo katika hali hii?

Chid Benz: Uvimbe huu ndio unasababisha, nisipobwia unaniuma mno, sasa huwa nautuliza kwa kuvuta.

NDANI YA CHUMBA CHAKE HOTELINI

Baada ya maongezi ya muda mrefu, Chid aliwaamini wageni wake kiasi cha kuwakaribisha chumbani kwake, kwa ajili ya kuendelea na mazungumzo. Chumbani, OFM walishangaa kumuona Chid akitoa mfuko chini ya godoro, ambao ndani yake kulikuwa na sigara, wembe, kipande cha kigae, mirija na kopo la soda lenye maji nusu, likiwa limetobolewa na mrija kupitishwa.

Baada ya kutoa vifaa hivyo, Chid alikaa na kutoa kete za madawa ya kulevya na kuanza kuandaa kwa ajili ya kubwia. Huku akichukuliwa picha za video kwa uhodari wa hali ya juu bila kufahamu, mara mbili alishtukia kuwa anarekodiwa.

Lakini hata hivyo, kila aliposhtuka, alipoozwa kwa maneno matamu ya stori zikaendelea hadi saa tisa usiku.

OFM: Sasa Chid kwa nini hutaki kuachana na haya madawa wakati watu mbalimbali wanajaribu kukusaidia?

CHID: Aaah, nishawaambia ninaumwa, hata watu wanaonisaidia wamekwisha niambia niendelee tu kutumia taratibu lakini nijali uhai nisizidishe nisije kufa.
GPL.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. M.mungu atamsaidia

    ReplyDelete
  2. Mungu atamsaidia"Mungu alisema jisaidie nami nitakusaidia yaani kwa mfano siyo umekurupushwa na simba karibu yako kuna mti halafu unamuomba Mungu akupandishe juu ya mti kitu ambacho hakitowezekana inatakiwa uupande mti naye atakupa nguvu ili uiepuke hiyo hatari ya kuliwa au kujeruhiwa na simba na siyo vingenevyo

    ReplyDelete

Top Post Ad