DR. Magufuli Yuko Sahihi na Serikali yake, Watu Walizoea Dezo Sana Tubadilike Jamani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Juzi hotuba ya Mh.Rais kuna baadhi ya watu wanaiponda, mimi nashangaaa sana hivi watanzania tukoje? Nchi hii jamani tulifikia pabaya sana kwa serikali kuendeshwa kwa ghiliba, uongo, udanganyifu, unafiki, na kupakaziana bila kuwa wakweli, tukaomba tumpate Rais atakae kuwa mkweli, asiyeogopa lawama za ndugu, marafiki, na wananchi ili tusonge na kutoka tulipo.

Juzi Mh.Rais akiwa Kagera amewaambia wanakagera, waanga wa tetemeko na wananchi kwa ujumla ukweli uliyomchungu na usiopingika kuwa serikali haiko kwa ajili ya mtu mmoja mmoja bali kwa maslahi ya jumla ya wananchi wote.

Sisi watanzania tulikuwa tumezoea sana maisha malaini sana, ya msaada, tegemezi na kulialia na kununa, mfn. mtu akiwa mfanyakazi anakuwa na tegemezi wengi sana mjini na kijijini wote wanataka salary yake ika wengine sasa hawafanyi kazi kisa kaka,dada,mjomba n.k yupo bandari, tra,tanesco n.k kila mtu sasa afanye kazi na siyo kumtegemea mtu au mambo ya kona kona ili usawa uwepo na nchi isongeee. Nchi inaendelea kwa kuwa na producers wengi, sisi tuna production man-force kubwa ila wategeaje na wazembe.

Ifike wakati sasa ukweli usemwe hata kama ni chungu na ina kera kiasi gani. Awamu iliyopita watu walipenda kusikia uongo na maneno ya kuremba na kubembelezwa.

By Leo Ojije/JF
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Oiiii!wasiomuelewa Shauri zao,tetemeko ni kama mafuriko,Moto.watasaidiwa wangapi?Muhimu ,chakula matibabu.wakuwaangalia hapo NI wazee,yatima na kama Kuna walemavu wasiojiweza.

    ReplyDelete
  2. Kahama/shinyanga waliahidiwa kujengewa nyumba baada ya mafuriko tangu 2013/2014 kimyaaaaaaaa mpaka leo,je tuendelee kudanganywa?Bora kusema ukweli japo wachache watalaaumu.

    ReplyDelete
  3. SIKU ZOTE UKWELI UNAUMA.

    ReplyDelete

Top Post Ad