11 Jan 2017

Emmanuel Mbasha Atoboa Siri ya Flora Mbasha Kuzaa Nje ya Ndoa...Adai Bado Anamuitaji Warudiane

Msanii wa muziki wa Injili, Emmanuel Mbasha amesema bado anamuhitaji aliyekuwa mke wake Flora Mbasha ingawa anadai tayari ameshazaa nje ya ndoa na mwanaume mwingine.

Muimbaji huyo amedai ameshafanya jitihada mbalimbali bila mafanikio kwa kipindi cha miaka miwili ili kurudiana na mama watoto wake huyo.

“Moyo wa kurudiana nilikuwa nao sana, tena sana, ikiumbukwe mambo yametokea 2014, mwaka huo mzima nilikuwa namuomba Flora rudi nyumbani tuendelee na maisha, 2015 nikaendelea kumuomba rudi nyumbani tuendelee na maisha. Tumeitisha vikao vya kila aina ili kusuluishwa lakini bado amekuwa mgumu lakini nadhani tayari alishapanga haya yatokee ndio maana akaamua yeye kuniacha mimi nilikuwa sina mpango huo,” Emmanuel Mbasha alikimbia kipindi cha Enewz cha EATV..

“Mimi sijaachana naye, sema tumetengana na kipindi tumetengana amepata mtoto labda kuna kitu anaogopa, lakini mimi sina tatizo naye, Flora mimi nakuhitaji rudi nyumbani tuendelee na maisha,” aliongeza.

Muimbaji huyo alishinda kesi ya ubakaji iliyokuwa ikimkabili baada ya Mahakama kuthibitisha muimbaji huyo hakuwa na hatia.

Kesi hiyo ilifunguliwa na mke wake huyo akimtuhumu aliyekuwa mume wake huyo kumbaka binti yatima ambaye walikuwa wanaishi naye.

Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD


Share:
Weka Maoni yako Hapa

3 comments:

  1. HAH!! MTU ALIYETAKA UFUNGWE MAISHA BADO UNAMTAKA??? DUU I CANT BELIEVE!!!!

    ReplyDelete
  2. Mimi pia siamini kuwa kweli Emmanuel ametamka ujinga kama huo hilo malaya lilitaka ufungwe jela maisha, kakusingizia kuwa umebaka leo hii unataka kumrudia? Au hela zimeisha benk ndiyo maana unataka kumrudia, maana zilivuma tetesi kuwa Emmanuel alikuwa anachukua hela zote za Flora anajiwekea kwenye akaunti yake ndiyo maana Flora akamuacha akaenda kuzaa na jamaa mwingine

    ReplyDelete
  3. Mziki wa injili umeshatiwa doa.... hawa wawili dah

    ReplyDelete

Total Pageviews


Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger