Hatua Nne Za Kujifunza Kutokana Na Makosa.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mara nyingi tumekuwa tukisema ili ufanikiwe ni muhimu sana kujifunza kutokana na makosa. Tumekuwa tukiongea sana kuhusu juu ya hilo mara kwa mara na kukusisitizia juu ya umuhimu wake.

Pamoja na msisitizo huo wa kujifunza kutokana na makosa ambao tumekuwa tukikupa, leo tumeona vyema tukuongezee kitu cha cha ziada katika huko kujifunza kutokana na makosa.

Kitu hiki si kingine bali hatua ambazo unatakiwa uchukue ili uweze kujifunza kwa makosa kiuhakika. Kwa kujifunza hatua hizi itakusaidia wewe  kuvuka hapo ulipo na kwenda ng’ambo nyingine kimafanikio.

Ili kunielewa vizuri katika hili hebu twende pamoja tuangazie nukta kadhaa zitakazo tusaidia kuzielewa hatua nne za kujifunza kupitia makosa tunayoyafanya kila siku kwenye maisha yetu.

Hatua 1.  Andika makosa yako.

Unapojikuta upo katika kitu kipya unachofanya, tambua makosa yapo na ni lazima utafanya. Kitu cha kwanza cha kufanya ili uweze kujifunza vizuri kutokana na makosa yako, andika makosa yako. Hakuna mkato katika hili, andika makosa yako ili ikusaidie wapi pa kuanzia pale unapotaka kujirekebisha. 

Hatua 2. Jifunze kutokana na makosa ya wengine.

Usisubiri sana kujifunza kutokana na makosa yako, angalia pia wengine wanafanya makosa gani, pia yachukue makosa hayo na ya andike mapema ili yasije yakajirudia na kwako pia.  Unapoandika makosa ya wengine mnaofanya kitu kinachofanana inakusaidia na wewe kuwa makini sana.

Hatua 3. Andaa orodha ya makosa ya kuyafanyia kazi.

Katika hatua ya kwanza na ya pili utakuwa umefanya zoezi la kuandika makosa yako. Hapa katika hatua hii andaa sasa makosa ambayo unataka kuyafanyia kazi lakini ambayo yametoka kwenye orodha uliyoandika kwenye hatua mbili zilizotangulia, kisha chukua hatua.

 Hatua 4. Hakikisha usiridhike mapema.

Hata mara baada ya kurekebisha makosa yako, usibweteke na kuridhika na kujiona wewe ni wewe. Endelea kujifunza kutokana na makosa mengine tena na tena na kurudia hatua hizo, hiyo itakufanya uzidi kuwa bora sana siku hadi siku
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad