Hii Noma Sana..!! Prof Lipumba Awachafua Mbowe na Lowassa Jukwaani,Amewashutumu Kwa hili..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi(CUF) Profesa Ibrahimu Lipumba amewataka wananchi wa kata ya Isage kutomchagua kiongozi katika ngazi ya udiwani kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa kuwa wanaweza 'wakamuuza' kama walivyofanya kwa Dk Wilbroad Slaa kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita.

Ameyasema hayo jana katika mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombe wa chama hicho, Saidi Juma uliofanya ndani ya kata ya Isagehe Wilayani hapa Mkoani Shinyanga.

Lipumba alisema Chadema ilipitisha Dk Slaa kuwa mgombea urais, lakini Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe alimuuza kisha kumpatia nafasi hiyo aliyekuwa Waziri Mkuu wa awamu ya nne, Edward Lowassa.

“Msichague viongozi wapiga dili kwani mkimchagua diwani anayetoka Chadema naye anaweza kuuzwa kama Mwenyekiti wao wa Taifa, Freeman Mbowe alivyomuuza Dk Slaa uchaguzi mkuu uliopita mkaanza kuhangaika kutafuta maendeleo, chagueni kiongozi atakayesimamia rasilimali za wanaisagehe,” amesema Lipumba.

Pamoja na mambo mengine, Lipumba alisema wananchi wanatakiwa kuchagua kiongozi bora atakayetambua changamoto za wanaisagehe ikiwa ni pamoja na kusimamia rasilimali za wananchi na kuongeza kuwa kufanya hivyo itafanya kata hiyo kupata maendeleo ya haraka.

“Kama wananchi mtamchagua Diwani wenu kupitia chama cha CUF ,basi nitatoa ushauri wa mara kwa mara juu ya kunyanyua uchumi wa kata hii ili kuleta maendeleo ya haraka kwa wananchi… binafsi ni mtaalamu wa kutafuta wafadhili bahati nzuri shule ya Isagehe ilijengwa na kanisa la pentekoste Sweden hivyo naweza kuwaunganisha nao,” amesema.

Mgombe wa kiti hicho cha udiwani, Saidi Juma alisema atahakikisha anatekeleza yale yote aliyosema wakati wa kampeni ikiwa ni pamoja na kumshirikisha Profesa Lipumba katika kumshauri namna ya kuongoza kata na kutafuta wafadhili ili kata ipate maendeleo ya haraka.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad