SBL inalaani Kusambazwa Kwa Video isiyo na Maadili Kwenye Mitandao ya Kijamii

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

TAARIFA KWA UMMA

Dar es Salaam Januari 12, 2017- Kampuni ya Bia ya Serengeti inapenda kuwataarifu wateja wake na  umma na kwa ujumla kuwa kuna  video isiyo na maadili   inaiyosambazwa katika mtandao ya kijamii ikionesha msanii akiigiza  na kuimba wimbo wenye  mahadhi ya taarabu  mbele ya bango lenye nembo ya bia Serengeti Premiur Lager.

Tunapenda kuweka bayana kuwa onesho la msanii huyo halikuidhinishwa wala kudhaminiwa na SBL Pia  msanii huyo sio sehemu na hajawahi kuwa mmoja wa mawakala wetu wanaotoa huduma za kutangaza bidhaa zetu.


Video hiyo ambayo haizingatii maadili ya sanaa  inatoa picha mbaya  jambo ambalo ni kinyume na sera ya SBL ya kuzingatia maadili mema katika shughuli za kutangaza bidhaa zake. 

Aidha ikumbukwe kwamba SBL imekuwa mstari wa mbele  katika kulinda na  kusimamia maadili katika shughuli zake  za kijamii  ikiwa ni pamoja na kuhamasisha  unywaji wa pombe kistaarabu.

Tunauhakikishia umma na wateja wetu kuwa  SBL inafanya shughuli zake za kijamii kwa kuangalia mambo yenye tija kwa jamii na sio vinginevyo.

Tunapenda kuwashukuru sana wateja wetu na umma kwa ujumla kwa kuendelea kushirikiana nasi.

Imetolewa na 

Mkurungezi wa Mahusiano
Serengeti Breweries Limited.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad