Kama Una Stress, Pitia Hapa! Usiache Kutupia na Wewe Maneno Yako!..!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kuna vijimisemo vifupi vimeibuka huku kwenye mitandao kwa sasa, yaani ni full burudani!
Ukivisomo mwisho lazima ubaki mdomo wazi au ucheke, baadhi ya niliyokutana nayo naweka hapa, pia karibuni kwa wenye zaidi tuburudike pamoja!

Leo kidogo nipigwe na MWANAMKE baada ya LIFTI kusimama...wakati tupo kwenye lift Nilikua nayaangalia MAZIWA yake akasema "Bonyeza Moja" mi si nikalibonyeza?
Yaani had sasa
bado najiuliza nilipokosea.

Hivi Utajisikieje Utakaposikia Rafiki Yako wa Karibu Hajaja Kwenye Mazishi Yako ???!
Nadhani Mimi Sitamwongelesha Tena !!!! 
I think nakaribia kupona

Nimenunua chips ili nile kwa bahat mbaya mtoto wa mama mwingine amekaa next to me akaanza kuzililia.
Imebidi nivae earphones. Napenda watoto, ila utoto ndio sipendi..

Jana nimepita njia ya mkato makaburini warembo wawili wakawa wananikimbilia wanatetemeka Eti tunaogopa kupita peke yetu na mm Nikawajibu hata mm nilivyokuwa hai nilikuwa naogopa sana . Wakazimia
Sipendagi kufatwa fatwa mm

Ex wangu leo kaupdate status yake ya watsap et "NILIOTEMBEA NAO WOTEMKAPIME" Saizi nipo apa pa fundi nguo pana foleni sanaHarusi sijui lini anapenda kushtukiza sana

Niliwahi kusikia kuwa maji na mafuta havichangamani, na pia mafuta huwa yanaelea juu ya maji... Basi jana mimi nikaamua kupaka mafuta mengi tu miguuni kisha nikaingia baharini ili niweze kutembea juu ya maji maana nilihisi ningeelea na kuweza kufanya chochote.
Sikumbuki nini kilitokea lakini nilijikuta nimelala mchangani watu wakiwa wamenizunguka huku wakisema niwashukuru sana wavuvi. Nadhani watakuwa wamenipa samaki wa bure.

Leo nimeenda kuchangia damu hospitalini,mara wananambia soda na biskuti zimeisha..!
Sa hii nipo zangu njiani na damu yangu kwenye blood bag naelekea nyumbani. Bora niwapelekee mbu take away..

Mwalimu kaniulizaa kama mtoto mdogo anaitwa mchanga... Je mtu mkubwa anaitwaje? ... Nikamjibu anaitwa kokoto..... Ameniitaa staff room labda atakuwa ameniitia chai

Huyu mwalimu ana roho nzuri sio kama mwl Msigwa

Stress ni nini??
Stress ni pale umeenda kijijini kwa bibi ako huku umebeba jeans zako tano zile ja mtindo wa kuchanika (chanika jeans) sasa siku ukazifua ukazianika ukaenda zako kutembea ile unarudi jioni unakuta bibi yako kazianua afu kazishona zote!
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad