MREMBO Lulu Diva na Uhusika Wake Katika Madawa ya Kulevya..

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Lulu Diva, mrembo anayefanya muziki wa Bongo Flava ambaye alitajwa kwenye orodha ya watu wanaodaiwa kuhusika na madawa ya kulevya amezungumzia alivyochukulia na jinsi wazazi wake walivyojisikia.

Akiongea na Bongo5, mrembo huyo amesema hakutarajia kutajwa kwenye orodha hiyo na ni kitu ambacho kiliwashtua mpaka ndugu zake kwa kuwa hajawahi kujihusisha na biashara hiyo haramu.

“Nilishtuka kwa sababu ni kitu ambacho sikuwahi kutarajia wala kutegemea kwa kuwa nilikuwa sifahamu chochote. Nilivyosikia vile nilikosa raha kabisa niliumia lakini namshukuru Mungu by the way,” amesema.

“Bado inaniaffect kwa kuwa ni itu ambacho hujawahi kutegemea, huhusiki wala hujawahi kufanya kwa hiyo kitu kama kile kinakuumiza pale unapokuwa unakutana na watu ambao hawafahamu halafu huwezi kusema unamkalisha mtu uanze kumpa somo umuelezee,” ameongeza.

Lulu amedai kuwa mpaka leo hii taarifa za tukio hilo hazijaweza kumfikia mama yeke kwa kuwa yupo mbali ambaye anaishi mkoani Tanga na kipindi alikuwa anajua mwanae kasafiri kwakuwa alishamuaga tangu muda mrefu.

“Mama yangu mpaka leo hakuwahi kufahamu kwa sababu the time niliyokuwa nimetajwa nilikuwa natarajia kusafiri kwahiyo akawa anajua mimi nimesafiri. Na vile kwa sababu yupo mbali hakuwahi kupata taarifa mapema lakini kwa ndugu zangu ndio iliniaffect sana kwa sababu wenyewe pia wanashangaa kwa sababu wapo na mimi muda mwingi na wanajua jinsi walivyonikuza na wananielewa vizuri mtoto wao. Kwa hiyo ilikuwa pia surprise na waliangalia vitu vingi kwa wao wenyewe kwa baadhi ya watu kuwalaumu.”

Kuhusu kulala rumande kwa siku tano, Lulu amesema, “Kipindi kile mule ndani sikuhitaji rafiki, yaani nilikuwa nasali nakesha nikiomba Mungu ili ukweli ujulikane ili nije kutoka mule ndani,” amesema.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad