STEVE Nyerere : Naomba radhi kwa viongozi wote niliowataja kwenye mazungumzo yangu na mama sepetu.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Msanii wa Filamu na Muigizaji mahiri hapa nchini Steve Nyerere, akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar kuhusiana na mambo mbalimbali yaliyotokea hivi karikuni ,likiwe suala la ujumbe wa sauti ambao umekuwa ukisambazwa katika mitandano ya kijamii ukimuhusisha yeye Steve pamoja na Mama Wema Sepetu.

Katika Mkutano huo STEVE NYERERE amesisitiza kuwa kilichosemwa na WEMA SEPETU kuwa anaidai CCM fedha ni uongo, kwani walilipwa huku akisema Msanii aliyelipwa fedha nyingi katika kazi hiyo ni Wema Sepetu, hivyo anashangaa kusikia akidai kuwa hajalipwa.

Mradi wa Mama Ongea na Mwanao uliratibiwa na Steven Nyerere huku akisaidiwa na Wema Sepetu na kazi yake ilikuwa ni kutoa elimu kwa wazazi kuwa karibu zaidi na vijana wao wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Hata Hivyo, Steve Nyerere, ametumia mkutano huo kukiri kuwa Sauti iliyotumwa kwenye Mitandao ya Kijamii inayohusisha mazungumzo yake na Mama yake Wema Sepetu ni ya kwake, hivyo amewaomba radhi viongozi wote aliowataja katika mazungumzo hayo.

'Kulikuwa na maongezi ya simu kati ya mimi na mama Sepetu, mimi ndio nilikuwa naogea na mama Sepetu yasipindishwe,"Ile Sauti imekuja kuachiwa juzi wakati watu wanahama chama, kwanini nirekodiwe? naamini wamefanya hivyo makusudi" ,alisema Steve Nyerere

"Namuomba radhi Rais Magufuli na Chama changu cha CCM, yanaongelewa mengi ninayasikia, naomba radhi familia pia, niliteleza,Nimetaja viongozi katika ile sauti halafu mtu anakuja kuisambaza nimetaja viongozi wa Nchi, Mama alichofanya amenikosea sana,Lakini namuachia Mungu"alimaliza kusema
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. NDO FUNDISHO, MJIFUNZE KUACHA MAJUNGU NA UONGO

    ReplyDelete
  2. you are very funny yaani sina la kusema jamani sauti ni yako na ulikuwa unaobgea vizuri na kwa mapenzi kwa kum support wema yaani niseme kwa kifupi hujakosea kitu kwa nini uomve msamaha na yaliomkuta wema yes ni uonevu sana tu ni uko wazi kabisa jamani ogopeni mungu ukweli kawaida uanauma dont fear kuongea ukweli socwhy ujifanye unaomba msamaha for what?

    ReplyDelete
  3. Sasa yaliyosemwa ni ukweli au. Je kama si mtu wa kujulikana nani atakutoa kama umebambikizwa kosa. Wangapi wapo magerezani kwa tuhuma zisizo sahihi. Na kwa vipi chama kinaingilia kati kumsaidia mtu mmoja. Toka maraisi, mawaziri, wabunge. Hii inaonyesha wazi sheria inachagua, inapendelea , na kunamambo yanasukwa.Hapa haitumiki sheria moja wazi kwa kosa moja. serikali inachagua yupi wa maana tumsafishe, mwacheni mtu wa kawaida hana maana. Na hii ndiyo vita kuu kati ya Upinzani na chama tawala. Uhaki, Ukweli, usawa, na sheria kutenda kazi ipasavyo.

    ReplyDelete

Top Post Ad